Kuendelea kwa kongamano la kitamaduni la kipindi cha Karbala awamu ya tano katika jiji la Islamabad

Maoni katika picha
Miongoni mwa program za wiki ya kitamaduni ya kipindi cha Karbala, inayo simamiwa na Atabatu Husseiniyya tukufu katika nchi ya Pakistan na kushiriki Atabatu Abbasiyya, katika siku ya pili iliyo sadifiana na siku ya Ijumaa ya tarehe: 16 Machi 2018m, sawa na 27 Jamadal-Thani 1439h, ugeni wa ataba mbili tukufu ulitembelea mji wa (Bahriyataun), miongoni mwa waliopokea ugeni huo ni Imamu na khatibu wa Ijumaa wa Masjid Jaamia Khadijatu Kubra Shekh Zaahid Hussein Zuhdi na kundi kubwa la wakazi wa mji huo miongoni mwa wapenzi wa Ahlulbait (a.s), walipewa zawadi ya bendera ya Imamu Hussein (a.s), nao waliikumbatia kwa ajili ya kufanya tabaruku na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kutokana na jina la bwana wa mashahidi, pendera imewasili na kupepea katika mji huu ikiwa na manukato kutoka katika ardhi takatifu ya Karbala, baada ya hapo ugeni ukashiriki katika swala ya Ijumaa, halafu Sayyid Muhammad Ali Halo kutoka katika hauza ya Najafu Ashrafu akapewa nafasi ya kuongea, miongoni mwa aliyo sema ni:

Ni fahari kubwa kwetu leo hii kua pamoja na ndugu zetu katika mji huu mtukufu ambao alama za kuwapenda watu wa nyumba ya Mtume (a.s) zinaonekana wazi.

Akaongeza kusema kua: Tupo katika siku za kukumbuka kuzaliwa kwa bibi Zaharaa (a.s), karibu na kuingia mwezi mtukufu wa Rajabu ambao ndani ya mwezi huo kuna uzawa wa maimamu watakasifu watatu, mwanzoni kuna uzawa wa Imamu Baaqir (a.s) na uzawa wa Imamu Ali Haadi (a.s), na katikati ya mwezi huo kuna uzawa wa kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s), ndugu zangu yatupasa kuzitumia tarehe hizo tukufu kwa kuchota elimu na maarifa kama kweli tunataka kufuata mwenendo sahihi wa dini tukufu.

Akaendelea kusema kua: Hakika kongamano hili na vikao hivi vitukufu, vitatufaa siku ambayo haitamfaa mtu mali yake wala watoto, vikao hivi ni kuhuisha mambo ya Ahlulbait (a.s), na kufanya hivi ni miongoni mwa vielelezo vya kufaulu siku ya kiyama, tunamuomba Mwenyezi Mungu atukutanishe kwa Muhammad na Aali Muhammad rehma za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake na Aali zake, na mwisho wa maombi yetu tunasema Alhamdu lilaahi Rabil-Aalamina.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: