Kamati ya maandalizi ya kongamano la kimataifa kuhusu kuhuisha utengenezaji wa historia na kuiandika: Hauza ya Najafu Ashrafu ilikua na nafasi muhimu katika maktaba ya historia…

Profesa Haadi Abdunabi Tamimi
Katika hafla ya kufunga kongamano la kimataifa kuhusu uhuishaji wa kutengeneza historia na kuiandika iliyo fanyika siku ya Ijumaa (27 Jamadal-Thani 1439h) sawa na (16 Machi 2018m), kulikua na ujumbe wa kamati ya maandalizi ulio wasilishwa na Profesa Haadi Abdunabi Tamimi, miongoni mwa aliyo sema ni:

“Hakika umma huchukua historia yake na hubaki unakumbuka yaliyo pita na kuangalia athari za yaliyo fanywa na mababu zao, pamoja na kilicho andikwa na kalamu katika mambo mbalimbali, pengine umma wetu wa kiislamu na kiarabu unaweza kua miongoni mwa umma zilizo piga hatua, watoto wema wa umma huu wameonyesha kujali turathi na historia, kwa kuzama ndani ya vitabu na kutafuta ukweli wa matukio, jambo la kuchambua na kuhakiki limekua ni moja ya kazi zao kielimu, kazi ambayo haikua rahisi, ilikua na hatari kubwa kutokana na aina ya utawala ulio kuwepo, kwani ulikua ni utawala unao ficha ukweli na kuzua mambo”.

Akaongeza kua: “Ilianza kuandikwa historia ya Mtume mtukufu kisha yakatokea yaliyo tokea, matukio muhimu yakapotoshwa, hali ikaendelea hivyo hadi kufikia katika historia ya sasa, uandishi wa historia sio jambo rahisi, hakuna anaye weza kupambana na mitihani ya kazi hiyo ispokua mtu mwenye imani kubwa na msimamo imara wa kuvumilia mateso na matatizo, kutokana na umuhimu wa jambo hili, hauza ya Najafu iliona umuhimu wa kupambana na watawala na kutekeleza wajibu wao, wakafanya kazi kubwa ya kukusanya vitabu vya historia vya kila zama za hatua za histori kuanzia matukio ya kihistoria hasa yaliyo tokea katika miji mitakatifu”.

Akabainisha kua: “Kwa ajili ya kuweka wazi kazi kubwa iliyo fanywa na hauza ya Najafu Ashrafu, Atabatu Abbasiyya tukufu na taasisi ya Bahrul-Uluum Al-Khairiyya, wameamua kuanzisha safari hii ambayo mwaka huu tumefika katika kituo cha tatu kwa kufanya makongamano ya kielimu na kimataifa, ambapo safari hii tumeangalia nafasi ya hauza ya Najafu Ashrafu katika kutengeneza historia na kuiandika, na kwa ajili ya kusisitiza mchango wao katika kutunza taarifa za matukio ya sasa bila kuyapotosha na kuyaharibu”.

Tamimi akaendelea kusema kua: “Kutokana na msingi huo na kwa taufiq ya Mwenyezi Mungu, kamati ya maandalizi ya kongamano hili kwa muda wa miezi kadhaa imekua ikitoa mialiko kwa wasomi mbalimbali, miongoni mwa wanachuoni watafiti walio tumia kalamu zao kuandika tafiti madhubuti zilizo wasilishwa ndani ya siku mbili za kongamano hili, jumla tulipokea tafiti (70) zilizo elezea mada sita za kongamano, kutokana na uchache wa muda pamoja na kufanana kwa baadhi ya tafiti ilitulazimu kuchagua tafiti chache na bora zaidi katika hizo, kwa kutumia kamati maalumu iliyo zipitia na kuchagua hizi zilizo wasilishwa kwenu kwa muhtasari baada ya kukidhi vigezo vyote vya kielimu”.

Akamaliza kwa kusema kua: “Tunaomba radhi kwa kuacha baadhi ya tafiti kutokana na kutoendana na mada za kongamano zilizo tangazwa, Mwenyezi Mungu ni shahidi, hakika tulisoma kwa umakini mkubwa tafiti zote, ili tusimdhulumu yeyote katika kazi kubwa ya kielimu aliyo fanya, tunaomba radhi kwa upungufu wowote uliojitokeza kwa wageni wetu au kama kuna jambo lolote tulilisahau hata kama ni dogo kiasi gani”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: