Huu ndio muhtasari wa watafiti wa kongamano la kimataifa kuhusu kuhuisha utengenezaji wa historia na kuiandika...

Dokta Mushtaqu Abbasi Muan
Kongamano la kimataifa kuhusu kuhuisha utengenezaji wa historia na kuiandika, lililo fanyika chini ya kauli mbiu isemayo (Hauza ni kitovu cha mabadiliko), linalo simamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na taasisi ya Bahrul-Uluum Al-Khairiyya, limetoka na maazimio yaliyo wasilishwa na mjumbe wa kamati ya maandalizi Dokta Mustaqu Abbasi Muan katika hafla ya kufunga kongamano iliyo fanyika alasiri ya siku ya Ijumaa (27 Jamadal-Thani 1439h) sawa na (16 Machi 2018m), na hii ndio nakala ya maazimio hayo:

Mwisho wa kongamano letu yatupasa kutambua sababu muhimu za kufanywa kwa kongamano hili, tambueni kua lengo kuu lilikua ni kuangalia umuhimu wa kutunza historia yetu ya sasa kwa ajili ya kuwarahisishia vizazi vijavyo waweze kujenga umma unao nufaika na uzowefu wa watu waliopita ili waweze kujiepusha na makosa na kufika kwa amani, kuna tofauti ya wazi baina ya kusoma historia na kuiandika upya na jukumu kubwa tulilo kua tukisisitiza la kusoma historia kwa umakini na kubaini matukio kwa kuchambua sehemu za makosa na athari zake kwa ajili ya kujiepusha nayo, jambo ambalo linasaidia kurekebisha umma wa sasa na kujenga mustakbali mwema, kupitia orodha ya tafiti zilizo jadiliwa katika kongamano hili na maoni yaliyo tolewa na watafiti pamoja na wahudhuriaji watukufu, tumefanikiwa kutengeneza maazimio ambayo tumeyaandika kwa ufupi katika nukta zifuatazo:

Kwanza: Kuendeleza mawasiliano ya kielimu kati ya hauza na taasisi za elimu za sekula ikiwa ni pamoja na vyuo vikuu na vituo vya elimu, kwa ajili ya kujenga kukamilishana kielimu ili kufikia kuhuisha utengenezaji wa historia na kuiandika.

Pili: Kuangalia athari za fatwa za Marjaa dini na mchango wake katika kutengeneza historia, hususan katika masomo ya sekula yanayo husika na historia ya Iraq ya sasa na ya kale, na kuangalia kwa mazingatio hatua za ukoloni wa Mwingereza katika mwaka wa 1941m hadi kubadilishwa kwa utawala mwaka 2003m na kipindi cha Daesh mwaka 2014m na vipindi vingine.

Tatu: Malalo tukufu katika kipindi chote zimekua chanzo cha maelekezo mengi ya matukio ya kihistoria, kwa hiyo tunawazindua watafiti watilie umuhimu kufuatilia matukio hayo kihistoria.

Nne: Tuna wasisitiza watafiti wafuatilie athari za hauza katika kujenga uchumi na athari yake katika hatua mbalimbali za historia.

Tano: Kufanya juhudi ya kusoma historia na kuisahihisha, tunatamani watafiti wabainishe uzushi na upotoshwaji uliojaa katika historia yetu, hususan iliyopo katika selibasi za masomo kutokana na athari yake kwa umma.

Sita: Kufanya juhudi ya kutafsiri yaliyo andikwa na watafiti wa kiarabu kuhusu historia ya hauza na wanachuoni wake katika lugha zingine ambazo zipo hai, ili kuujulisha ulimwengu mafanikio hayo.

Saba: Wizara ya utamaduni ya Iraq, ifungue kitengo cha (Darul Kutub wal wathaaiq) kitakacho kusanya taarifa na kuzihifadhi zinazo husiana na historia ya Iraq ya sasa, hususan kuanzia mwaka wa 2003m.

Nane: Tunatarajia kongamano lijalo lizungumzie upatikanaji wa hauza ya lugha ya kiarabu na fani zake, na mada za kongamano zizungumzie yanayo tokea katika Qur’an tukufu kwa kupatikana hauza za kielimu.

Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: