Atabatu Abbasiyya tukufu na taasisi ya Bahru-Uluum Al-Khairiyya zahitimisha kongamano la kimataifa kuhusu kutengeneza historia na kuiandika…

Maoni katika picha
Alasiri ya Ijumaa (27 Jamadal-Thani 1439h) sawa na (16 Machi 2018m) lilihitimishwa kongamano la kimataifa kuhusu uhuishaji wa kutengeneza historia na kuiandika, linalo simamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na taasisi ya Bahrul-Uluum Al-Khairiyya chini ya kauli mbiu isemayo: (Hauza ni kitovu cha mabadiliko) lililo fanyika siku mbili na kuhudhuriwa na wasomi wa hauza na sekula kutoka ndani na nje ya Iraq.

Hafla ya ufungaji wa kongamano hilo iliyo fanyika katika ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) ilihudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na katibu mkuu Muhandisi Muhammad Ashiqar pamoja na viongozi wa taasisi na wale wa Ataba tukufu.

Katika kikao cha ufungaji wa kongamano kamati ya maandalizi iliwasilishwa ujumbe wake kupitia Profesa Haadi Abdunabi Tamimi, miongoni mwa aliyo sema ni: “Hakika umma huchukua historia yake na hubaki unakumbuka yaliyo pita na kuangalia athari za yaliyo fanywa na mababu zao pamoja na kilicho andikwa na kalamu katika mambo mbalimbali, pengine umma wetu wa kiislamu na kiarabu unaweza kua miongoni mwa umma zilizo piga hatua..”

Konamano lilifungwa kwa kuwasilishwa orodha ya maazimio ya kongamano, yaliyo somwa na Dokta Mushtaqu Abbasi Muan, na mwisho kabisa zikatolewa zawadi kwa washiriki.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: