Chini ya kauli mbiu isemayo: Kuzaliwa kwa mtukufu… kwang’risha fani asilia, na kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Swidiqah Kubra Fatuma (a.s), kitengo cha malezi na elimu ya juu cha Atabatu Abbasiyya tukufu kinafanya maonyesho ya hati za kiarabu na kazi za ubunifu kwa shule za Ameed.
Maonyesho hao, yanafanyika ndani ya sardabu (ukumbi) wa kiganja (kafu) wa Ataba tukufu, yalianza asubuhi ya Juma Mosi (28 Jamadal-Thani 1439h) sawa na (17 Machi 2018m), na kuhudhuriwa na mjumbe wa kamati kuu ya uongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu Ustadh Adnaan Mussawiy, na Muhandisi Jafari Saidi pamoja na rais wa kitengo cha malezi na elimu ya juu Profesa Abbasi Didah, na msaidizi wake Profesa Mushtaqu Ali, na Dokta Jaasim Ibrahimi, na Ustadh Majidi Rabii pamoja na mkuu wa mkoa wa Karbala Ustadh Abbasi Audah.
Mjumbe wa kamati kuu ya uongozi Muhandisi Jafari Saidi Jafari, alionyesha furaha yake na akapongeza kufanyika kwa makongamano ya aina hii kwa kusema Makua: “Tunawapongeza ndugu zetu wa kitengo cha malezi na elimu ya juu kwa kufanya maonyesho ya kiufundi, hususan mradi wa hati za kiarabu kwa wanafunzi wa shule ambazo tunatarajia ziandae warithi wa fani hizi, hakika ni jambo la kufurahisha kuona matokeo kama haya kwa wanafunzi wa shule za Ameed yanayo ashiria mustaqbali mwema”.
Amma rais wa kitengo cha malezi na fani ya hati za kiarabu na michoro ya kiislam Dokta Misaa Khafaji amesema kua: “Maonyesho ya kiufundi awamu ya pili yana hatua tatu, (hatua ya kwanza ni watumishi wa kitengo cha elimu, hatua ya pili ni ya walimu wanao fundisha katika shule za Ameed, na hatua ya tatu ni ya wanafunzi wa shule za Ameed), akafafanua kua lengo la maonyesho haya ni kuibua vipaji vya wanafunzi na kuviendeleza sambamba na kuboresha uwezo wao kielimu”.
Mkuu wa malezi na ufundi Ustadh Abdulkarim Shimri akaoneza kua: “Maonyesho haya tumeyagawa sehemu tano, kuna sehemu maalum ya hati za kiarabu na michoro ya kiislamu, na sehemu maalum ya maumbo na vyombo vya mapambo, sehemu maalim ya kazi za mikono na sehemu ya tano ni kwa ajili ya kuonyesha mradi wa kufundisha hati mbalimbali za kiarabu, unao tekelezwa na shule za Ameed, idadi ya vitu vilivyopo katika maonyesho ni zaidi ya 300, ambavyo ni mbao za hati na michoro na kazi za kiufundi pamoja na kazi za mikono”.