Kutokana na makubaliano ya kushirikiana kielimu baina yao: Chuo kikuu cha Alkafeel chafanya kikao cha kujadili kazi ya mwanafunzi wa elimu ya juu wa chuo kikuu cha Fardusi…

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu ya Atabatu Abbasiyya tukufu asubuhi ya Juma Mosi (28 Jamadal-Thani 1439h) sawa na (17 Machi 2018m) wamefanya kikao cha kujadili kazi ya mwanafunzi wa elimu ya juu/ Masta, bwana Ahmadi Abdurazaaq Fatalawi / kitivo cha uhandisi – chuo kikuu cha Fardusi.

Kikao hiki kimefanyika kutokana na makubaliano ya kushirikiana kielimu na kitamaduni baina ya chuo kikuu cha Fardusi kilichopo (Mashhadi tukufu/ Jamhuri ya kiislamu ya Iran) na chuo kikuu cha Alkafeel, kikao cha mjadala huo kiliundwa na: Profesa Hamidi Ridha Abu Ridha makamo rais wa kitivo cha uhandisi katika chuo kikuu cha Fardusi, mwenyekiti wa kikao, na Dokta Saidi Kamalidini Ghiyathi, mkufunzi wa kitivo cha uhandisi katika chuo kikuu cha Fardusi, mjumbe, Profesa Aabidina Wahidiyani makamo rais wa chuo kikuu cha Fardusi, mjumbe na msimamizi, Dokta Naswiru Qassim Hamudi rais wa kitengo cha uhandisi na ufundi wa kompyuta katika chuo kikuu cha Alkafeel, mjumbe na msimamizi.

Mwanafunzi mtahiniwa (mhojiwa) bwana Ahmadi Abdurazaaq Fatalawi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Mimi ni mwanafunzi wa kwanza kujadiliwa kazi yangu baada ya makubaliano ya chuo kikuu cha Alkafeel na Fardusi, nawashukuru viongozi wote wa vyuo hivi, na shukrani ya pekee iwaendee Atabatu Abbasiyya tukufu na uongozi wa chuo kikuu cha Alkafeel kwa msaada wao endelevu kwa kila mwanafunzi, kazi yangu ilikua inahusu kamera za ulinzi, hususan wakati wa ziara zinazo hudhuriwa na mamilioni ya watu za Imamu Hussein (a.s), kwa kutumia kurusha ndege zisizo kua na rubani, kupitia kamera hizo utaweza kuona sehemu yenye tatizo la usalama au jambo lolote linalo tokea”.

Mkuu wa chuo kikuu cha Alkafeel Profesa Nurus Muhammad Shahid Dahaan aliongeza kusema kua: “Chuo kikuu cha Alkafeel kiliingia mkataba wa kushirikiana na chuo kikuu cha Fardusi tangu miaka mitatu iliyo pita, miongoni mwa ushirikiano huo ni kuanzisha kitengo cha lugha, kikiwemo Kifarsi, na kutumia walimu walio bobea kutoka chuo kikuu cha Fardusi kwa ajili ya kukuza uwezo wa wanafunzi katika lugha ya kifarsi, chuo kikuu cha Alkafeel kimesha andaa utaratibu wa kutekeleza makubaliano hayo, na hii ni sehemu ya utekelezaji wa makubaliano, kwa kufanyika vikao vya kujadili kazi za wanafunzi wa elimu za juu, jambo linalo ongeza ushirikiano wa kielimu katika siku za usoni”.

Mjadala ulimalizika kwa mwanafunzi huyo –aliye soma digrii ya kwanza katika chuo kikuu cha Alkafeel/ kitivo cha uhandisi na ufundi wa kompyuta- kupata daraja la vizuri mno (mumtaaz).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: