Mwitikio mkubwa wa watu wanao kuja kutembelea matawi ya Ataba mbili tukifu katika maonyesho yanayo fanyika sambamba na kongamano la wiki ya kitamaduni awamu ya tao…

Maoni katika picha
Wiki ya msimu wa Karbala (Nasimu Karbala) inayo adhimishwa katika mji mkuu wa Pakistan Islamabad, nakusimamiwa na Atabatu Husseiniyya tukufu pamoja na ushiriki wa Atabatu Abbasiyya kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Al-Kauthar, miongoni vya vipengele vya mkusanyiko huu ni kufanyika kwa maonyesho maalumu ya Ataba mbili tukufu, matawi yanayo shiriki yamepata mwitikio mkubwa sana kutoka kwa watu wanaokuja kutembelea maonyesho hayo, nao wameonyesha vitu mbalimbali, Atabatu Abbasiyya tukufu imetenga sehemu maalumu ikaweka bendera ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ambayo imeandikwa: Ewe mwezi wa bani Hashim. Kwa ajili ya watu kufanya tabaruku, na wametenga sehemu ya pili kwa ajili ya kuonyesha machapisho ya kitengo cha habari na utamaduni, vikiwemo vitabu vya kimaadili na vya ziara, machapisho yote hayo yalilenga kuwanufaisha wadau, pia waligawa picha za kaburi na ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), pamoja na baadhi ya zawadi za kutabaruku, kama vile pete na mawe yaliyo chukuliwa katika kaburi tukufu pamoja na baadhi ya bendera zilizo fanyiwa tabaruku katika kubba tukufu, pia walikua na sehemu maalumu ya maonyesho ya picha za mnato (photography) zilizo pigwa na wapiga picha wa Ataba tukufu kwa utalamu wa hali ya juu, na zilikubalika sana na mazuwaru, pamoja na hayo, wamefunga screen kubwa kwa ajili ya kuonyesha matangazo ya moja kwa moja (mubashara) kupitia mtandao wa kimataifa Alkafeel, ambao una mlango maalum wa ziara kwa niaba, na wametenga sehemu ya watu kujisajili kwa ajili ya kutuma barua kwa Abulfadhil Abbasi (a.s).

Na kuhusu tawi la Atabatu Husseiniyya tukufu, nao pia wanavitu vingi, kuna sehemu ya kutabaruku na bendera ya kubba la Imamu Hussein (a.s), wanagawa zawadi za kutabaruku, na kuna kipengele cha kuandika barua kwa Imamu Hussein (a.s), vilevile wanaonyesha machapisho ya maktaba ya Imamu Hussein (a.s), ambayo yanamada 10 tofauti na zaidi ya nakala 30,000, wametengeneza sehemu maalumu ya picha za makaburi matukufu, pamoja na kugawa folda zinazo mtambulisha bibi Fatuma Zaharaa na bibi Zainabu Kubra (a.s), pia wanafafanua utukufu wa turba ya Imamu Hussein (a.s), miongoni mwa mambo muhimu katika maonyesho haya, kuna maonyesho rasmi ya hospitali ndogo inayo toa huduma kwa kusaidiana na baadhi ya madaktari wa Pakistan, wanawapima wagonjwa na wanao bainika kua na matatizo makubwa wanawapeleka katika hospitali kubwa, na huduma zote za matibabu zinatolewa bure, pia Darul Qur’an ina ushiriki mkubwa, wanafundisha usomaji sahihi wa surat Fat-ha pamoja na sura zingine, pamoja na kuonyesha harakati zao, ikiwa ni pamoja na kuelezea mradi wa mahafidh elfu moja, kuna tawi lingine linashughulika na watoto, nalo lina vitu vingi, wanafundisha Qur’an, wanafafanua kuhusu taqlidi (ufwasi) pamoja na kuonyesha mbao za picha mbalimbali. Pia kuna tawi maalum la wanawake linafanana na tawi la watoto, pia kulikua na tukio la kupanda mti ambao una picha za mashahidi wa vita tukufu ya kujilinda.

Kumbuka kua kongamano hili hufanywa kila mwaka katika jiji la Islamabad, na hupewa umuhimu mkubwa sana kutokana na athari yake katika nyoyo za watu, ukizingatia kua linawakurubisha na Ataba za mji mtukufu wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: