Muendelezo wa shughuli za wiki ya kitamaduni msimu wa Karbala katika nchi ya kiislamu Pakistan

Maoni katika picha
Shughuli za kongamano la msimu wa Karbala linalo simamiwa na Atabatu Husseiniyya tukufu kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Al-Kauthar na ushiriki wa Atabatu Abbasiyya zinaendelea, siku ya tatu ya kongamano hilo ambayo ni Juma Mosi 17 Machi 2018m sawa na 28 Jamadal-Thani 1439h, ugeni wa Atabatu mbili tukufu umeelekea kusini ya mji wa Islamabad, na kua wageni wa mji wa (Jakwal) katika kijiji cha (Dudiyal) ambacho kina taasisi ya elimu iliyo chini ya chuo kikuu cha Al-Kauthar, ujumbe wa Ataba mbili walipata nafasi ya kukagua harakati zinazo fanywa na taasisi hiyo.

Sehemu ya kwanza walitembelea shule ya Imamu Swadiq (a.s) ya wavulana, wakapokelewa na mkuu wa shule hiyo pamoja na walimu wa shule, baada ya kuwatembeza katika madarasa na kuwaonyesha selebasi za masomo, wageni walionyesha kufurahishwa na njia za kisasa zinazo tumika katika ufundishaji wa shule hiyo. Kituo cha pili wakaenda Masjid Jaamia (Mudhhiru Imaan) ambayo ipo chini ya uongozi wa chuo kikuu cha Al-Kauthar, wakapokelewa na uongozi wa msikiti pamoja na wanafunzi wanao soma msikitini hapo, walionyesha mapenzi makubwa katika mapokezi yao, katika ziara hii pakazinduliwa Maahadi ya kuhifadhisha Qur’an tukufu, uzinduzi huo ulikua na hafla kubwa, iliyo funguliwa kwa Qur’an tukufu iliyo somwa na muadhini wa Ataba mbili tukufu bwana Aadil Karbalai, baada ya hapo ukafuata ukaribisho wa wageni, halafu ukafuata ujumbe kutoka kwa wageni ulio wasilishwa na Sayyid Adnaan Jalukhaan Mussawiy, ambaye alisema kua: “Inatufurahisha sana kua pamoja na ndugu zetu wapenzi wa Ahlulbait (a.s) katika nchi ya Pakistan, wapenzi hawa ambao tumeona shauku yao ya kutaka kutembelea Ataba tukufu, hisia zao zinatokana na ukweli wa nia zao”.

Akaongeza kusema kua: “Tumekuja kutoka Karbala tukufu tukiwa tumebeba alama ya mapenzi kutoka katika ardhi ya Twafu, inayo maanisha utiifu na utekelezaji, nayo ni bendera ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ambayo leo inapepea sehemu kubwa ya dunia, hakika Abulfadhil Abbasi (a.s) alionyesha msimamo wa kishujaa na kibinadamu huko Karbala, jambo ambalo leo tunahitaji kulifanyika kazi sana”.

Akaendelea kusema: “Leo tupo mbele yenu enyi ndugu zangu wapenzi kuwakumbusha hadhi ya Abulfadhil Abbasi (a.s), mtu huyu anaheshima kubwa mbele ya maimamu watakasifu, kama tunavyo sema katika ziara yake, tunashuhudia unyenyekeviu na ukweli wake, hizi sifa mbili alikua nazo Abulfadhil Abbasi (a.s), alionyesha ukweli pale alipo kuja naye Imamu Abu Abdillahi Hussein (a.s), na akaonyesha unyenyekevu na utiifu pale alipo pigana kunusuru kiini cha uislamu hadi akafa shahidi, tunamuomba Mwenyezi Mungu atuwezeshe kuwapenda Ahlulbait (a.s) na awalinde wafuasi wao kote duniani hakika yeye ni msikivu na mjibuji”.

Kisha kikafuata kipengele cha usomaji wa Qur’an kukoka kwa mahafidh wa Darul Qur’an ya Atabatu Husseiniyya tukufu, na baada yake wahudhuriaji wakaenda kupandisha bendera ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika uwanja wa Masjid Jaamia (Madhharu Imaan).

Halafu wakaswali swala ya jamaa nyuma ya Sayyid Adnaan Jalukhaan Mussawiy Imamu wa jamaa katika haram tukufu ya Abbasi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: