Masunni wa mji mkuu wa Pakistan Islamabad washerehekea mazazi ya bibi Fatuma Zaharaa (a.s).

Maoni katika picha
Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zimeshiriki katika hafla zilizo andaliwa na (Jamiatu naimiyya lil-uluumi diniyya) huko Islamabad na ndugu zetu Masunni, ushiriki huu ni miongoni mwa ratiba ya wiki ya kitamaduni msimu wa Karbala (nasimu Karbala) awamu ya tano, hafla hiyo imehudhuriwa na wanachuoni wengi wa kisunni pamoja na wakazi wengi wa mji huo, kutokana na kushiriki kwa ugeni kutoka katika Ataba mbili tukufu, amboa umepata mapokezi makubwa kutoka kwa mkuu wa chuo na Imamu wa swala ya jamaa, hafla ikaanza kwa ujumbe kutoka kwa mkuu wa chuo Shekh Kalzaar Ahmadi Naiimi, ambaye alisema kua: “Tunafuraha kubwa kwa ujio wenu kutoka katika mji mtukufu wa Karbala, tunaona utukufu mkubwa kupata nafasi ya kuwahudumia, pia tunatoa pongezi kwenu kwa ushindi mkubwa mlio pata dhidi ya magaidi ya Daesh, tunaungana na nyie katika furaha hiyo, hakika Marjaa dini mkuu amethibitisha kua yeye ni kielelezo cha amani ya umma wote wa kiislamu na sio kwa Shia peke yake, ndio maana leo tunashirikiana, na huu ni ushindi mkubwa, tumefanya hafla kubwa ya pamoja kusherehekea mazazi ya bibi Fatuma Zaharaa (a.s).

Akasisitiza kua: “Hakika wanachuoni wa kishia wana nafasi kubwa katika kuunganisha umma wa kiislamu, hususan Shekh Muhsin Najafi, anafanya juhudi kubwa ya kuunganisha Wapakistan Sunni na Shia, anashirikiana na sisi katika kila kitu na anatwita kwake mara kwa mara”.

Akaendelea kusema kua: “Hakika kukumbuka kuzaliwa kwa Zaharaa na maimamu (a.s) kuna athari kubwa katika nafsi zetu, tunaona ni wajibu kwetu kuhuisha tarehe hizi, na hili jambo linatokana na msukumo wa itikadi yetu, hakika imani haikamiliki ispokua kwa kuhuisha kumbukumbu za Ahlulbait (a.s), kwa msingi huo ndio tunafanya hafla za aina hii, tunamuomba Mwenyezi Mungu awaunganishe waislamu na awaangamize wale wanaotaka kupanda mbegu ya fitna baina ya waislamu”.

Ukafuata ujumbe wa Mheshimiwa Sayyid Muhammad Halo kutoka katika hauza ya Najafu Ashrafu, ambaye alisema kua: “Tunawashukuru sana ndugu zetu masunni wa Islamabad kwa mapokezi mazuri mliyo tupa, ambayo yanatupa nguvu ya kuendeleza kampeni ya kuishi kwa amani, jambo linalo sisitizwa na Marjaa dini mkuu, na sisi tunakufikishieni salamu za Marjaa dini mkuu Sayyid Sistani, ambaye anatutaka kubeba jukumu la kuwasaidia ndugu zetu masunni..”. Akasisitiza kua: “Tunatamani kuona selebasi za kiislamu zikikataza ubaguzi na kusisitiza umoja, hili ni jukumu letu yatupasa tulifanye, ndio alivyo fanya kiongozi wa waumini (a.s), kwa utukufu wa Mwenyezi Mungu na kwa juhudi za wasimamizi wa kongamano la msimu wa Karbala mwaka wa tano na kwa nia zenu nzuri tunatarajia kufanikiwa kwa kazi hiyo Inshallah”.

Ujumbe mwingine ukawasilishwa na Shekh Munjid Kaabi kutoka katika Atabatu Husseiniyya tukufu, alibainisha kua: “Iko wazi kwenu ndugu zangu, hakika Mwenyezi Mungu mtukufu alipo leta Qur’an hakuihusisha na muda au sehemu moja, wala sio ya kundi fulani, bali inawahusu binadamu wote wa tabaka tofauti na dini mbalimbali, Qur’an ni muongozo wa Mwenyezi Mungu kwa waja wake wote unao waelekeza katika mambo mazuri yenye faida kwao”.

Akafafanua kua: “Ndugu zangu watukufu tunatakiwa kuacha tofauti zetu na kupambana na fikra potofu ambazo ni sumu inayo eneo baina yetu na kutaka kuua mwili huu mmoja kwa ajili ya kuzima mafundisho sahihi ya kiislamu, mwisho! Tunawashukuru sana kwa mapokezi mazuri, hakika nyie mnawakilisha madhehebi sahihi ya Sunni kwa sababu mmeshikamana na mafundisho sahihi ya uislamu mtukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: