Ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wawa mwenyezi wa mahafali ya Qur’an tukufu…

Maoni katika picha
Miongoni mwa hafla za Qur’an katika mradi wa (Arshi tilawah) kituo cha miradi ya Qur’an katika Maahadi ya Qur’an tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya wanafanya mahafali ya Qur’an ndani ya ukumbi mtukufu wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), pamoja na wasomaji wa mradi, wameshiriki pia wasomaji kutoka Iran miongoni mwa wageni wa mradi wa (wasomaji wa kitaifa).

Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na makomo waziri wa utamaduni na maelekezo ya kiislamu wa Iran Dokta Faqhiy Zaadah, ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu iliyo somwa kwa mahadhi ya kiiraq na Muhammad Abbasi Ahmad mwanafunzi wa mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa, kisha ikasomwa kwa mahadhi ya kiiran na Muhammad Swadiq Swarimiy mmoja wa wageni, kisha akafuatia msomi wa kimataifa kutoka Iran Wahidi Nadhriyaan, baada yake akasoma Ali Murtadha kutoka katika mradi wa kiongozi wa wasomaji, na mwisho akaingia msomi wa kimataifa wa Iran Haamid Ali Zaadah.

Mwisho wa hafla hiyo, wageni kutoka Iran wakapewa vyeti vya ushiriki, nao waliishukuru Maahadi ya Qur’an ya Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kuwapa nafasi ya kushiriki katika hafla ya Qur’an ambayo imefanyika ndani ya ukumbi mtukufu wa mwezi wa familia Abulfadhil Abbasi (a.s).

kumbuka kua mradi wa (Arshi tilawah) unao fanywa na kituo cha miradi ya Qur’an cha Maahadi ya Qur’an tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya, hufanywa jioni ya kila Ijumaa ndani ya ukumbi mtukufu wa haram ya Abbasi na hualikwa wasomi wa kimataifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: