Kituo cha uchapishaji Alkafeel chaonyesha utalamu wa hali ya juu katika matawi ya Atabatu Abbasiyya tukufu yanayo shiriki kwenye maonyesho ya kimataifa Bagdad…

Sehemu ya kazi ya kituo katika maonyesho ya kimata
Atabatu Abbasiyya tukufu inashiriki katika maonyesho mawili ya kimataifa yanayo endelea huko Bagdad, maonyesho ya wiki ya kilimo na maonyesho ya mambo ya afya (tiba), maonyesho yote yana ushiriki wa kitaifa na kimataifa, Ataba imewakilishwa na (Shirika la teknolojia ya kilimo, viwanda vya kisasa, kundi la vitalu vya Alkafeel, shirika la uchumi la Alkafeel na hospitali ya rufaa Alkafeel) kila tawi limeonyesha vitu vinavyo endana na hadhi ya maonyesho haya.

Kituo cha uchapishaji namba na utengenezaji wa matangazo, kilichukua jukumu muhimu la kubuni na kutengeneza sehemu za maonyesho katika ufanisi, ubora na muonekano mzuri wa kuvutia.

Kiongozi wa kituo hicho Ustadh Muhammad Aali Taajir ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kituo kimekua na uzowefu katika mambo haya, tumefanya kazi nyingi kutokana na ushiriki wa Atabatu Abbasiyya tukufu katika maonyesho mbalimbali na kila maonyesho yana uhusika maalumu, maonyesho haya ni kama sehemu ya ukamilishaji wa maonyesho yaliyo tangulia, matawi ya Ataba yanayo shiriki yamekua kivutio cha maonyesho kutokana na usanifu wa maonyesho yao, yametengenezwa kisasa na yana muonekano mzuri sana”.

Akaongeza kusema kua: “Baada ya kuafiki kushiriki katika maonyesho haya, na kwa mujibu wa maelekezo ya kamati inayo simamia maonyesho, tulichukua vipimo vya kila tawi shiriki, kisha tukaanza kusanifu sehemu ya kila tawi kutokana na aina ya vitu watakavyo onyesha, na kwa kutumia rangi zinazo ashiria uhusiano na Ataba tukufu, baada ya kumaliza kusanifu tukaingia katika hatua ya ujenzi ambayo tulitumia vifaa vya kisasa kabisa vinavyo endana na aina ya ujenzi wa kila tawi”.

Akabainisha kua: “Kazi yetu haikuishia hapo, tulitengeneza folda na vipeperushi vya utambulisho kwa kila tawi na tukaweka alama katika kila tawi ambazo haziathiri maonyesho, kisha tukatengeneza majukwaa ya matangazo”.

Akaendelea kusema kua: “Kazi hiyo ilidumu kwa siku kadhaa, alhamdu lilahi imekua kama ilivyo tarajiwa, kwa ushahidi wa watu wanao tembelea maonyesho hayo, matawi ya Atabatu Abbasiyya tukufu yamekua kama nyota zing’aazo katikati ya matawi haya lufufu, ukubwa wa eneo la matawi ya Atabatu Abbasiyya yanayo shiriki katika maonesho ya afya ni mita za mraba 64 huku matawi yanayo shiriki katika maonyesho ya wiki ya kilimo yakiwa na eneo la mita za mraba 52”.

Kumbuka kua kazi hii ilikua inaigharimu Atabatu Abbasiyya pesa nyingi sana, lakini sasa hivi kazi zote zinafanywa na kituo cha uchapishaji cha Alkafeel, na kina uzowefu na uwezo wa kutosha wa kufanya kazi hizi, kituo kinaweza kutoa huduma ndani na nje, katika mkoa wa Karbala na maeneo mengine, kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na ofisi ya kituo idara ya masoko iliyopo katika mkoa mtukufu wa Karbala kitongoji cha Hussein (a.s) barabara kuu, au piga simu kwa namba zifuatazo: (07602324000 – 07602322220 – 07702666550).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: