Hivi punde.. Ofisi ya Marjaa dini mkuu yatangaza kesho ni mwezi mosi Rajabu…

Maoni katika picha
Ofisi ya Marjaa dini mkuu Ayatullah Sayyid Ali Sistani imetangaza kua, kesho siku ya Juma Tatu (19 Machi 2018m) ni siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Rajabu (1439h).

Kutokana na mnasaba huo, mtandao wa kimataifa Alkafeel unawatakia heri na baraka watumishi wake wote kwa utukufu wa Abulfadhil Abbasi (a.s), tunamuomba Mwenyezi Mungu ajaalie mwezi huu na miezi mingine kua yenye heri nyingi na baraka kwa Iraq na raia wake pamoja na nchi za kiislamu hakika yeye ni msikivu na mjibuji.

Mwezi wa Rajabu ni mwezi wa Mwenyezi Mungu, ni miongoni mwa miezi mitukufu, nao ni mwezi wa kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s), unaitwa “Aswabu” kwa sababu Mwenyezi Mungu mtukufu humimina rehma zake kwa wingi ndani ya mwezi huu kwa umati wa Muhammad (s.a.w.w), nao ni mwezi wa kuomba msamaha (Istighfaar), katika siku ya kwanza kuna mambo yamesuniwa kufanywa, miongoni mwa mambo hayo ni:

Kwanza: Kufunga. Imepokewa kua Nabii Nuhu (a.s) alipanda safina yake katika siku hii, akawaambia walio kua pamoja naye wafunge, na atakaye funga siku hii atawekwa mbali na moto mwendo wa mwaka mzima.

Pili: Kuoga.

Tatu: Kumzuru Imamu Hussein (a.s), amepokea Shekh kutoka kwa Bashiri Dahaan kutoka kwa Swadiq (a.s) anasema: (Atakaye mzuru Hussein bun Ali (a.s) katika siku ya kwanza ya mwezi wa Rajabu Mwenyezi Mungu atamsamehe kabisa).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: