Umati mkubwa wajitokeza katika kufunga kongamano la msimu wa Karbala awamu ya tano…

Maoni katika picha
Program tofauti zilizo kuwepo katika kongamano la msimu wa Karbala awamu ya tano, ambalo husimamiwa na Atabatu Husseiniyya na kushiriki Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Al-Kauthar katika mji mkuu wa Pakistan Islamabad, Umati mkubwa wa viongozi wa dini na raia wa kawaida pamoja na wageni kutoka katika Ataba mbili tukufu wameshiriki ufungaji wa kongamano hilo jioni ya siku ya Juma Pili 18 Machi 2018m sawa na 29 Jamadal-Thani 1439h, hafla ya ufungaji wa kongamano ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu, iliyo somwa na muadhini wa Ataba mbili tukufu bwana Aadil Karbalai, baada yake ikafanyika program ya Darul Qur’an ya Atabatu Husseiniyya tukufu, halafu ukafuata ujumbe wa chuo kikuu cha Al-Kauthar ulio wasilishwa na Mheshimiwa Shekh Muhsin Ali Najafiy, ambaye amesema kua:

Kila sifa njema anastahiki Mwenyezi Mungu ambaye ametuandikia kuishi katika mazingira haya matukufu tukiwa na wageni kutoka katika ardhi ya Karbala, hii ni neema kubwa, ya kufikiwa na watumishi wa Ataba mbili tukufu, nao ndio waliofanya kila aina ya juhudi za kufanikisha kongamano hili tukufu, ambalo limekua likiwakunisha waislamu wa Pakistan kila mwaka, na kuwafanya wale ambao hawawezi kwenda Karbala wafanye ziara kupitia kongamano hili, hii ni miongoni mwa baraka za Imamu Hussein (a.s) kwetu, tunamuomba Mwenyezi Mungu azilinde Ataba tukufu na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) katika kila pembe ya dunia.

Kisha akaongea Mheshimiwa Sayyid Muhammad Halo kutoka katika hauza ya Nafafu Ashrafu, miongoni mwa aliyo sema ni:

Katika hafla ya kufunga msimu wa karbala, tunahisi kua ujumbe wa Imamu Hussein (a.s) umeshinda, alipo jitolea kitu chenye thamani zaidi kwake kwa ajili ya kulinda uislamu, na kufikisha ujumbe wake duniani kutokea Karbala, wa kwamba uislamu sahihi ni kushikamana na tabia za Mtume (s.a.w.w), tunawaahidi! Tutawaelezea watu wa karbala mazingira haya, na tuta watangazia kua watu wa Pakistan wana hamu kubwa na Imamu Hussein (a.s), kila mwananchi wa Iraq anakualikeni na yuko tayali kuwahudumia, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu atudumishe katika mapenzi ya Ahlulbait (a.s) hakika yeye ni msikivu na mjibuji.

Kisha akazungumza Sayyid Adnaan Jalukhaan Mussawiy kutoka katika Atabatu Abbasiyya tukufu, akabainisha kua:

Naona furaha kubwa katika nyuso za wahudhuriaji watukufu, na sisi tuna furahi kushirikiana na nyie katika furaha hii, inayo tafsiri mapenzi ya dhati kwa Ahlulbait (a.s), na sasa hivi tunaingia katika furaha nyingine ya kuingia mwezi mtukufu wa Rajabu, tunao uanza kwa kusherehekea kuzaliwa kwa Imamu Baaqir (a.s), aliye kamilisha ujenzi wa dini ya kiislamu, akafundisha wanachuoni wengi wakubwa katika uislamu, walio tufikishia turathi za Ahlulbait (a.s), katika mwezi huu kuna ibada nyingi, ikiwa ni pamoja na kumzuru Imamu Hussein (a.s), hususan tumekusanyika hapa kwa ajili ya kuitaja Karbala katika mazingira haya matukufu, tunamuomba Mwenyezi Mungu awawafikishe wasimamizi wa kongamano hili tukufu.

Mwisho kabisa akazungumza Shekh Munjid Kaabiy kutoka katika Atabatu Husseiniyya tukufu, ambaye alisema kua:

Tumeishi siku hizi tukufu, na tunapo hitimisha kongamano hili, hatuna budi kutoa shukrani kwa Imamu Hujjah (a.f) pamoja na wanachuoni wa kishia hususan wakazi wa mji huu, walio tupa nafasi ya kukutana chini ya mapenzi ya Imamu Hussein (a.s), mtu aliye rekebisha mwelekeo wa umma, akaujulisha uongo na upotoshaji baada ya kufutwa kwa uislamu halisi na watu wanao abudu dunia, yatupasa tusome kutoka kwake kupitia msimamo alio onyesha katika vita ya Twafu, mkusanyiko huu ni miongoni mwa faida za ujumbe wa Twafu na athari ya ujumbe huo katika nyoyo zetu, tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutupa neema zisizo hesabika, na tunamuomba awalinde waislamu wa dunia nzima na awalinde wasimamizi wa kongamano hili.

Katika hafla hii, wanafunzi wa chuo kikuu cha Al-Kauthara walio hitimu masomo ya dini walivishwa vilemba, kisha wageni kutoka katika Ataba mbili wakapewa zawadi, halafu ikafanyika kura kwa ajili ya kuwapata watu watakao bahatika kwenda kufanya ziara katika Ataba tukufu za Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: