Miongoni mwa ratiba ya kushiriki katika program za vyuo vikuu, Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha habari na utamaduni, imeshiriki katika kongamano la kitamaduni linalo simamiwa na chuo cha Imamu Hussein (a.s) katika mkoa mtukufu wa Karbala kuanzia (17-19 Machi 2018m), chini ya kauli mbiu isemayo: (Tunaendelea kwa elimu, na tunamuiga Hussein, na tunajitolea kwa ajili ya Iraq).
Ushiriki ulikua wa aina mbili, kwanza: kushiriki katika hafla ya ufunguzi. Pili: kushiriki katika maonyesho ya vitabu yanayo fanywa sambamba na kongamano hilo, wameonyesha shehena kubwa ya machapisho ya kitengo hicho, vitabu na majarida mbalimbali, pamoja na machapisho ya kidini, kimalezi na kijamii zikiwemo picha za mnato na kazi zingine za kitaalamu.
Mkuu wa chuo hicho Dokta Jaasim Muhannah amesifu ushiriki wa Atabatu Abbasiyya tukufu na akasema kua, ni sehemu ya kujenga uhusiano na watu wa nje vikiwemo vyuo vikuu, jambo ambalo lina umuhimu mkubwa, pia ni fursa ya kuangalia machapisho ya Ataba tukufu na kujua miradi yake.
Kumbuka kua ushiriki huu ni miongoni mwa mkakati wa Atabatu Abbasiyya tukufu wa kujitangaza katika taasisi zote za kijamii hususan taasisi za kielimu na vyuo vikuu, imesha fanya makongamano mbalimbali katika vyuo tofauti vya Iraq, maonyesho hayo huhusisha machapisho yake na harakati zake katika sekta tofauti, katika maonyesho haya wamepata mwitikio mkubwa kutoka kwa wanafunzi na walimu.