Kuzaliwa kwa Imamu Baaqir (a.s): nuru yaangaza mbinguni, Malaika wapongezana kwa kuzaliwa Imamu muahidiwa…

Maoni katika picha
Siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Rajabu umma wa kiislamu hukumbuka kuzaliwa kwa nuru ya tano ya Muhammadiyya Imamu Muhammad bun Ali Baaqir (a.s), aliye pata mapema elimu ya watu wa mwanzo na wamwisho, alizaliwa mwaka wa (57h), akapokelewa na watu wa nyumba ya Mtume kwa furaha kubwa, kwani walikua wanamsubiri kwa muda mrefu kutokana na kubashiriwa na Mtume (s.a.w.w) kwa miaka mingi, akitokana na kizazi kitakasifu chenye utukufu na ukamilifu, watu wa familia hiyo ni vinara wa utukufu katika kila sekta, ukamilifu wa kibinadamu, akili, imani, upole na tabia njema.

Imamu Muhammad Baaqir (a.s) ni Imamu wa kwanza mtakasifu anaye tokana na maimamu wawili, yeye ni bun Imamu Ali Zainul-Aabidina bun Imamu Hussein mjukuu wa Mtume, bun Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s), huu ni upande wa baba yake. Amma upande wa mama yake, ni bibi mtakasifu Fatuma binti wa Imamu Hussan bun Ali bun Abu Twalib (a.s) na huitwa “Ummu Abdillahi”, alikua katika wanawake bora wa bani Hashim, Imamu Zainul-Aabidina alikua akimwita Swidiqah, Imamu Abu Abdillahi Swadiq (a.s) anasema: (Swidiqah hajapatikana katika familia ya Hassan mwanamke bora kama yeye), yatosha fahari kwake kuitwa pande la damu ya mjukuu wa Mtume, na amelelewa katika nyumba ambazo Mwenyezi Mungu anataka zitukuzwe, miguu ya mama huyu mtakasifu ndio iliyo mlea Imamu Baaqir (a.s).

Kuniya yake: (Abuu Jafari), hakuna mwingine anaye itwa kuniya hiyo zaidi yake.. amma laqabu zake tukufu (majina ya sifa) ni: (Amin, Shabihi (kwa sababu alikua anafanana sana na babu yake Mtume –s.a.w.w-) Shaakir, Haadi, Swaabir, Shaahid, Baaqir –na hili ndio jina mashuhuri zaidi-) pia jina hilo anaitwa yeye pamoja na mtoto wake Imamu Swadiq kama (Baaqirain) pia huitwa kwa jina la (Swaadiqain).

Imamu Baaqir (a.s) alisoma kwa baba yake Imamu Zainul-Aabidina (a.s), hadi akafikia kiwango cha juu kabisa cha elimu, akawa kama alivyo elezewa na babu yake Mtume (s.a.w.w) aliye mpa jina la Baaqir pale alipo sema: (Hakika atafanya haraka kupata elimu) alipo wabashiria waislamu kuzaliwa kwake na kwamba atakua na nafasi kubwa ya kuhuisha elimu ya sheria katika zama ambazo umma wa kiislamu utakua umetawala maeneo mengi, na kutakua na mchanganyiko wa tamaduni tofauti, wakati wote uislamu unajulikana kwa ufasaha wa kuongea na hoja za nguvu katika mijadala ya kifiqhi na mantiki na katika maswala ya hukumu za kisheria, alikua anawafundisha wanachuoni wa zama zake, walio kua wanafunga safari kwenda kumuuliza maswali mbalimbali na kujadiliana naye na kunufaika naye (a.s).

Imamu Muhammad Baaqir umri wake wote aliishi katika mji wa Madina, na alikua anafundisha umma wa kiislamu, alikua anasimamia kundi jema lililo anzishwa na Mtume (s.a.w.w) na likalelewa na Imamu Ali kisha Imamu Hassan na Hussein (a.s), pia liliendelea kupata chakula cha roho kutoka kwa baba yake Ali bun Hussein (a.s) walio kua na kila aina ya ukamilifu na utukufu.

Imamu Baaqir (a.s) aliishi na babu yake Imamu Hussein (a.s) miaka mitatu na kidogo, na alishuhudia vita ya Karbala, kisha akaishi na baba yake Sajjaad (a.s) miaka thelathini na nane, akisoma utukufu kutoka kwa baba yake na namna ya kubeba ujumbe kutoka katika asili yake tukufu na kuufikisha kwa wanadamu, muda wa uimamu wake ulikaribia miaka ishirini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: