Katika ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) zasikika kaswida za kukumbuka kuzaliwa kwa Imamu Baaqir na Haadi (a.s)…

Maoni katika picha
Katika mazingira yaliyo jaa furaha ndani ya ukumbu wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kitengo cha mawakibu na maadhimisho ya Husseiniyya chini ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya kimefanya hafla kubwa kwa ajili ya kuhuisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Baaqir na Imamu Haadi (a.s), ambao walizaliwa ndani ya siku za kwanza za mwezi mtukufu wa Rajabu, ambao umeandama jioni ya jana Juma Pili.

Hafla hii ilikua ni kikao cha usomaji wa mashairi, na ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha washairi wakaanza kusoma beti za mashairi yaliyo onyesha mapenzi kwa Ahlulbait (a.s) hususan wahusika wa tukio.

Hali kadhalika hafla hii, iliyo pata mahudhurio makubwa kutoka kwa mazuwaru watukufu, ilishuhudia uimbaji wa kaswida za kimashairi zilizo jaa furaha na bashasha, na kutolewa kwa ahadi ya kufuata mwenendo wa Mtume na mawasii wake maimamu watakasifu (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: