Watafiti waangazia uhai wa Imamu Baaqir (a.s) kielimu katika kongamano la nne…

Sehemu ya kikao cha kiutafiti
Kongamano la kitafiti la Imamu Baaqir awamu ya nne lililo anza leo (1 Rajabu 1439h) sawa na (19 Machi 2018m) chini ya kauli mbiu isemayo: (Imamu Baaqir (a.s) ni tunu ya wasii na mrithi wa elimu ya Mtume), limeshuhudia uwasilishwaji wa mada za kitafiti kuhusu mazingira ya kielimu aliyo ishi Imamu Baaqir (a.s), kikao hicho kimefanyika ndani ya ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu na kuhudhuriwa na watafiti wa kisekula.

Baada ya kumaliza uwasilishwaji wa mada katika kikao cha ufunguzi wa kongamano, kulikua na kikao cha jioni kilicho ongozwa na Dokta Ahmad Swabihi Kaabiy, ambacho kilikua na watafiti wa kisekula kutoka ndani na nje ya mkoa mtukufu wa Karbala, mada zenyewe zilikua kama zifuatavyo:
Mada ya kwanza: Iliwasilishwa na Dokta Daudi Salmaan Khalf Zubaidi kutoka katika chuo kikuu cha Bagdad, kitivo cha (tarbiyatu Ibun Rushdi lil-uluumi insaniyya) mada yake ilikua inasema (Imamu Baaqir (a.s) na changamoto za zama zake, utafiti wa aina za changamoto na njia za kupambana nazo).

Mada ya pili: iliwasilishwa na Dokta Muhammad Naadhim Muhammad Mafraji rais wa kitengo cha fiqhi na usulu katika chuo kikuu cha Karbala, mada yake ilikua inasema (Imamu Baaqir (a.s) na nafasi yake katika elimu ya usulu).

Mwishoni mwa kikao hiki, kilicho hudhuriwa na watafiti wengi wa kisekula, kulikua na maoni na michango mbalimbali iliyo tokana na majibu pamoja na ufafanuzi wa mambo muhimu yaliyo hitaji kufafanuliwa zaidi na watoa mada.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: