Hivi ndio walivyo huisha watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) kuzaliwa kwa Imamu Baaqir (a.s)…

Maoni katika picha
Kwa baaqir Uluumi muhammadiyya na taa lake ling’aalo.

Kwa jua la maarifa ya Alawiyya na bahari yake yenye mawimbi makubwa.

Kwa msingi wa dini na bwana wa walimwengu.

Mioyo inaimba mapenzi na utawalishaji.

Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wamezowea kila siku ya Juma Tatu na Alkamisi kuonyesha mapenzi yao kwa Ahlulbait (a.s), lakini kuna siku zinakua na umaalumu wake, kama siku za kuzaliwa kwa maimamu watakasifu (a.s), ambayo imesadifiana na siku ya Juma Tatu ya kwanza ya mwezi wa Rajabu, siku ambayo umezaliwa mwezi wa tano miongoni mwa miezi ya Muhammadiyya, Maimamu waongofu! Imamu Muhammad Baaqir (a.s).

Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) walipo maliza kusoma ziara huku wamesimama kwa mstari mbele ya kaburi takatifu, wakiwa wamebeba maua kama ishara ya furaha yao katika kuhuisha tukio hili, huku wakiimba kaswida zilizojaa beti zinazo onyesha mapenzi na unyenyekevu pamoja na kutaja utukufu wa Imamu (a.s) na upande mwingine wakitoa pongezi kwa Abulfadhil Abbasi (a.s) kutokana na tukio hili tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: