Kuhitimisha ratiba ya kongamano la kitamaduni la Imamu Baaqir (a.s) na kamati ya maandalizi yasema litaendelea kufanywa kila mwaka na mada zake zitakua zinawasilishwa kwa kiarabu na kiengereza.

Sayyid Aqiil Abdulhussein Yasiri
Kutokana na kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu wa tano, Imamu Baaqir (a.s), na ndani ya eneo tukufu la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), Alasiri ya Juma Tatu (mwezi mosi Rajabu 1439h) sawa na (19 Machi 2018m) kongamano la kitamaduni la Imamu Baaqir awamu ya nne limefungwa, lililo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha habari na utamaduni, chini ya kauli mbiu isemayo: (Imamu Baaqir (a.s) ni tunu ya wasii (a.s) na mrithi wa elimu ya Mtume (s.a.w.w)). Katika ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu na kuhudhuriwa na wawakilishi na ugeni wa viongozi mbalimbali.

Hafla ya kufunga kongamano ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu, kisha ukafuata ujumbe wa kamati ya maandalizi ulio wasilishwa na makamo rais wa kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Aqiil Abdulhussein Yasiri, baada ya kutoa pongezi kwa wahudhuriaji alisema kua: “Fahari yangu ni kuona sisi wafuasi na wapenzi wake tunahuisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwake na kuangalia nukta muhimu katika maisha yake, japo kua jambo hili ni gumu kwa wanadamu wote, kwa sababu historia yake na ya baba na watoto wake wema (a.s) hakuna mwanadamu anaye weza kuielezea na akaipa haki yake, tunajaribu tu kuogelea katika kina kirefu cha bahari, kisicho patikana chote hakiachwi chote”.

Akaongeza kusema kua: “Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu umefanya juhudi ya kuhakikisha inahuisha tukio hili tukufu kwa kufanya kongamano linalo endana na hadhi ya muhusika wake, ukawaomba wasomi wa dini watukufu na watafiti waandike mambo mema kuhusu mtukufu huyu”.

Akabainisha kua: “Idara ya Atabatu Abbasiyya tukufu inatoa wito wa kuendelea kufanyika kongamano hili kila mwaka kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, tunawaomba wasomi na watafiti muendelee kuandaa mada zenu tukufu kwa ajili ya kuwasilishwa katika kongamano lijalo, na mnaweza kuandaa kwa lugha ya kiarabu na kiengereza, ili tuwe na idadi kubwa ya mada za kitafiti kuhusu kiongozi wetu Imamu Baaqir (a.s)”.

Akaendelea kusema kua: “Hakika jambo hili tukufu lisinge kamilika kama sio ulezi mwema wa kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na katibu mkuu Muhandisi Muhammad Ashiqari pamoja na wajumbe wa idara husika na marais wa vitengo vya Ataba tukufu pamoja na kila aliye changia mafanikio haya, Mwenyezi Mungu awalipe kila la kheri”.

Pia akatoa shukrani kwa “Wahudhuriaji na wageni watukufu pamoja na wasomi na watafiti kutoka ndani na nje ya Karbala kutokana na michango yao kwetu, na akaomba samahani kwa kasoro yeyote iliyo jitokeza, kawaida samahani hukubaliwa na watu watukufu”.

Akamaliza kwa “Kutoa shukrani za dhati kwa wale ambao kuwashukuru ni wajibu wetu, watu wa Hashdi Sha’abi watukufu, ambao kama sio msimamo wao imara tusinge weza kufanya makongamano na nadwa na wala tusinge ishi kwa amani na utulivu, Mwenyezi Mungu awarehemu mashahidi zao wema na awaponye haraka majeruhi wote wa Hashdi Sha’abi na wa jeshi la serikali”.

Mwisho kabisa wa kongamano hili, watafiti walio wasilisha mada na wale walio changia kufanikisha kwa kongamano wakapewa vyeti na midani ya ushiriki.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: