Kongamano hili linafanywa kwa mara ya sita mfululizo chini ya usimamizi wa Atabatu Abbasiyya tukufu na kwa kusaidiana na kitengo cha lugha katika chuo kikuu cha Bagdad kitivo cha Ibun Rushdi cha elimu ya kibinadamu, kupitia kongamano hili na nadwa ndio ambavyo hutengeneza uhai wa mwanadamu na kumjulisha maimamu wake watakatifu, leo tunasherehekea ushindi wa Hashdi Sha’abi ambao ni mwendeleza wa ushindi wa mapambano ya Imamu Hussein (a.s), mapambano ambayo yameandikwa mara nyingi japo yalikua ya muda mfupi baada ya kutolewa fatwa na Marjaa mkuu Mheshimiwa Sayyid Ali Sistani, yaliyo zuia kuongezeka magaidi katika miji mingine ya Iraq, na yakazuia mjama za wasio itakia heri Iraq, kama sio kujitolea kwa majemedari wa jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi watukufu na kusimama kwao imara dhidi ya magaidi hoa Iraq yote ingekua chini ya udhibiti wa magaidi wa Daesh.
Baada yake ukafuata ujumbe wa rais wa kitengo cha lugha ya kiarabu Dokta Khalidi Hawidi, naye akasema kua:
Kitengo chetu kinafanya kongamano hili kwa mwaka wa sita mfululizo, na limetusaidia kuimarisha uhusiano na chuo, kwani ni ukurasa muhimu wa elimu ya sekula unao zungumzia swala la Imamu Hussein (a.s), kongamano hili linafanywa katika kipindi muhimu sana, kipindi cha ushindi dhidi ya magaidi wa Daesh, ambao wameleta shida na dhiki katika miji yetu kwa muda wa miaka minne, lakini majemedari wa Iraq watukufu wa jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi (wapiganaji wa kujitolea) wamefanikiwa kumshinda adui huyu na kumuondoa katika ardhi ya Iraq ambayo alitaka kuiteka, natoa wito kwa wanafunzi wote hasa wa kitivo cha Ibun Rushdi kitengo cha lugha ya kiarabu waweke picha za mashahidi katika vifua vyao, hakika wao ndio watu wanaofaa kuwekwa vifuano.
Akaongeza kusema kua: Katika kongamano hili la sita tumekusanya tafiti (35) kutoka katika vyuo vikuu tofauti vya Iraq, kamati ya elimu imepasisha tafiti (25), na mwisho natoa shukrani za dhati kwa ndugu zetu wa Atabatu Abbasiyya tukufu wasimamizi wa kongamano hili tangu lianzishwe hadi leo.
Kongamano lilikua na mada tatu za kielimu:
- 1- Mada ya kwanza: Khutuba za Twafu/ masomo katika majengo ya lugha na fani zake.
- 2- Mada ya pili: Hashdi Sha’abi katika khutuba ya Marjaa katika mizani ya lugha na fani zake.
- 3- Mada ya tatu: Upande wa maadili na akhlaq na utekelezwaji wake katika Hashdi Sha’abi.
Kongamano likahitimishwa kwa kugawa midani na vyeti kwa watafiti walio shiriki, pia wawakilishi wa Atabatu Abbasiyya nao wakapewa vyeti vya ushiriki.