Atabatu Abbasiyya yawekwa mapambo meusi kwa ajili ya kukumbuka kuuawa kishahidi kwa Imamu Ali Haadi (a.s)…

Maoni katika picha
Yeye ni msafi na ataendelea kua msafi na mbele ya Mola wake ni mridhiwa.

Aliuawa shahidi katika nyumba ya ugenini kwa shida uchungu na mateso.

Aliliwa na macho ya wema na uongofu kwa kuanguka bendera yake tukufu.

Aliliwa na jicho la anga izungukayo ikimuhuzunikia muongozaji na waongozwaji.

Aliliwa na babu yake mteule hadi weupe wa jicho lake ukatoweka.

Aliliwa na macho matukufu ya baba zake wema.

Imetanda huzuni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na kuta zake zimewekwa mapambo meusi kama ishara ya huzuni katika kumbukumbu ya kuuawa kishahidi kwa Imamu Ali Haadi (a.s), zimepandishwa bendera za kuomboleza, na kuwekwa vitambaa vilivyo andikwa maneno ya kuashiria huzuni ndani ya ukumbi wa haram tukufu kutokana na mnasaba huu mchungu, na kumuomboleza Mtume na watu wa myumbani kwake (a.s).

Kama kawaida ya Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba rasmi ya maombolezo, ambayo ina mambo mbalimbali, pamoja na utoaji wa mihadhara ya kidini na kufanya majlis za kuomboleza kutokana na ukubwa wa msiba huu.

Kumbuka kua mawakibu (misafara) ya kuomboleza tangu asubuhi ya leo imekua ikimiminika katika malalo ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ajili ya kutoa taazia na kumpa pole Imamu wa Zama (a.f), hali kadhalika huzuni imetanda katika Atabatu Abbasiyya na yamewekwa mapambo meusi katika ukumbi wa haram yake tukufu na bendera zinazo ashiria maombolezo zimepandishwa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: