Usiku wa Raghaaibu ni usiku wa Ijumaa ya kwanza ya mwezi wa Rajabu, una maana gani, utukufu gani na imesuniwa kufanya nini katika usiku huo?

Maoni katika picha
Mwezi wa Rajabu ni miongoni mwa miezi bora na mitukufu, zimepokewa riwaya nyingi kutoka kwa Mtume na watu wa nyumbani kwake (a.s) kuhusu utukufu wa mwezi huu na ulazima wa kuuheshimu, hakika ni mwezi wenye baraka kubwa, Mtume (s.a.w.w) anasema: (Rajabu ni mwezi wa kuomba msamaha kwa umati wangu, ombeni msamaha kwa wingi hakika yeye ni mwingi wa kusamehe na mwingi wa rehma. Na mwezi huu huitwa mmiminika (aswabu) kwa sababu rehma za Mwenyezi Mungu humiminika kwa wingi ndani ya mwezi huu, fanyeni wingi wa kusema: “naomba msamaha kwa Mwenyezi Mungu na ninamuomba toba”).

Kuna ibada nyingi ambazo zimesuniwa kuzifanya na zikasisitizwa kwa waumini, miongoni mwake ni; usiku wa kwanza wa Ijumaa ya mwezi wa Rajabu huitwa usiku wa Raghaaibu, Mtume (s.a.w.w) anasema: (…Msighafirike na usiku wa kwanza wa Ijumaa katika mwezi huu –mwezi wa Rajabu- hakika usiku huo Malaika huuita kua ni usiku wa Raghaaibu, kwa sababu inapo fika theluthi moja ya usiku huo, Malaika wote wa mbinguni na ardhini hukusanyika katika Kaaba na pembezoni mwake, na Mwenyezi Mungu huwaambia: enyi Malaika wangu niombeni mnacho taka, nao husema: ewe Mola wetu shida yetu kwako uwasamehe wafungao mwezi wa Rajabu, Mwenyezi Mungu huwaambia: nimesha fanya hivyo).

Usiku wa Raghaaibu: maana yake ni usiku wa kutoa sana, usiku huu unaheshima kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu, hutoa thawabu mara dufu kwa mtu atakaye funga mchana wake na akaswali usiku wake na akasoma dua na kufanya mambo mema, katika usiku huu wafungaji na wenye kuomba msamaha hukubaliwa maombi yao, ndipo Malaika wakauita usiku wa Raghaaibu.

Mtume (s.a.w.w) anasema: (Hakuna: Ibada muhimu zaidi kwa mja katika usiku huu kushinda, kufunga siku ya Alkhamisi ya kwanza ya mwezi wa Rajabu, kisha aswali baina ya Maghribi na Ishaa rakaa kumi na mbili, atakapo maliza aniswalie mara sabini, aseme: Allahumma swali alaa Muhammad wa alaa Aalihi, kisha asujudu na aseme katika sajda yake mara sabini: Subuuhu Quduusu Rabbu Malaaikatu wa Ruuhu, kisha akitoka mwenye sijda aseme: Rabbi-ghfir war ham watajaawaz ammaa taalam Innaka anta aliyyul aadham, kisha asujudu na kusema kama alivyo sema mwanzo, kisha amuombe Mwenyezi Mungu shida yake katika saijda yake, hakika Mwenyezi Mungu alamkidhia).

Kisha Mtume (s.a.w.w) akasema: (Naapa kwa haki ya yule ambaye nasfi yangu ipo katika uwezo wake, hataswali mja yeyote au umma wowote swala hii ispokua Mwenyezi Mungu atawasamehe madhambi yote hata kama yakiwa mengi kama povu la bahari, na atapewa nafasi ya kuwaombea watu mia saba katika familia yake waliokua wamehukumiwa kuingia motoni…).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: