Maahadi ya turathi za Mitume (a.s) ya masomo ya hauza ya kielektronik yatangaza kuanza kwa usajili wa masomo ya tamhidi…

Maoni katika picha
Maahadi ya turathi za Mitume (a.s) ya masomo ya hauza ya kielektonik chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza kuanza kwa usajili wa masomo ya tamhidi (maandalizi) ya kuingia katika masomo ya hauza ya kielektronik, usajili upo wa aina mbili:

Kwanza: Kujisajili rasmi na shule (kwa kukaa darasani).

http://www.edu.turathalanbiaa.com/create_student_account
pili: Kujisajili kwa kua msikilizaji (elimu masafa).

http://www.edu.turathalanbiaa.com/create_listener_accountbaada Baada ya kujisajili unatakuwa kupeleka kopi za vielelezo vifuatavyo:

  • 1- Kitambulisho cha uraia.
  • 2- Utambulisho au chiti cha shule (awe amemaliza sekondari kwa uchache)
  • 3- Barua ya utambulisho kutoka kwa Muutamad Marjaiyya mkuu wa eneo anapo ishi muombaji, mfano wa barua hiyo unapatikana katika anuani hii: https://t.me/informtionforturathalanbiaa

Kuhusu wakina dada wanaopenda kujiunga na masomo haya, wawasiliane na idara ya wanawake au watuandikie kupitia anuani za mtandao hizo hapo juu, baada ya kupokea vielelezo vyao vitapelekwa katika ofisi ya wanawake ya Maahadi, masomo yataanza (1 Shawwal 1439h).

Kumbuka kua Maahadi ya turathi za Mitume (a.s) ya maomo ya hauza ya kielektronik, ina uzowefu mkubwa katika swala la masomo ya hauza kielektronik, inatoa masomo hayo kwa wanafunzi wa kiume na wakike kutoka kila kona ya dunia, masomo yanayo fundishwa ni, Fiqhi, Aqida, masomo ya Qur’an tukufu, hukumu za usomaji na tajwidi, pamoja na masomo ya lugha ya kiarabu na Mantiki, vilevile wanafundisha Fiqhi ya wanawake, ibada ya hija, pia wanafunzi hupewa mazingira mazuri ya kujadiliana na walimu wao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: