Katika muendelezo wa miradi ya Qur’an: Maahadi ya Qur’an tukufu yazindua mradi wa kuendeleza vipaji vya Qur’an na yasisitiza kua ni sehemu ya ukamilishaji wa miradi iliyo tangulia na itajitahidi kufikia malengo…

Maoni katika picha
Katika muendelezo wa miradi ya Qur’an inayo lenga kuongeza uwezo na kukuza vipaji vya usomaji wa Qur’an, pamoja na kujifunza kila kitu kipya kinacho ingia katika uwanja wa Qur’an, kituo cha miradi ya Qur’an kilicho chini ya Maahadi ya Qur’an tukufu ya Atabatu Abbasiyya, kimezindua mradi mpya uitwao (Mradi wa kukuza vipaji vya usomaji wa Qur’an), mradi huu umefunguliwa kutokana na kuingia kwa mwezi mtukufu wa Rajibu.

Mradi! Utakua na semina pamoja na warsha mbalimbali katika maeneo tofauti zitakazo simamiwa na walimu walio bobea katika fani za Qur’an kutoka ndani na nje ya Iraq, warsha hizo zitahusisha vitu vifuatavyo:

  • 1- Sababu za msingi za usomaji wa Qur’an katika mwezi wa Qur’an.
  • 2- Njia mpya za ufundishaji.
  • 3- Utaratibu wa darsa za sauti.
  • 4- Uendeshaji wa mahafali na ratiba za vipindi vya Qur’an vya kwenye redio na luninga (tv).

Mradi umeanza na wanafunzi (60), wenye uwezo mzuri wa kusoma Qur’an tukufu kutoka katika Maahadi na matawi yake yaliyopo katika mikoa tofauti ya Iraq.

Shekh Jawadi Nasrawi mkuu wa Maahadi ya Qur’an tukufu ametuhadithia kua: “Tumezindia mradi huu kama sehemu ya kukamilisha miradi iliyo tangulia, na tutautekeleza kwa kufuata mkakati tulio jiwekea na kuhakikisha tunafikia malengo tarajiwa, tutatumia uwezo wetu wote kwa ajili ya kufanikisha hili, mradi huu unafanywa kwa mara ya kwanza, unalenga kukuza vipaji vya usomaji wa Qur’an, hatua ya kwanza itahusisha wasomaji wa Maahadi ya Qur’an na matiwi yake, hatua zijazo kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu zitajumuisha taasisi zote na Qur’an za hapa Iraq, kama sehemu ya kukitumikia kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu, chini ya walimu bora kutoka ndani na nje ya nchi”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: