Kwa ushiriki wa watafiti walio bobea: Kituo cha turathi za Karbala chafanya nadwa ya kielimu kuhusu turathi za Karbala tukufu…

Maoni katika picha
Chini ya kauli mbiu isemayo: (Turathi za Karbala katika uchunguzi wa wana sekula), Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu kituo cha turathi za Karbala kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Kufa asubuhi ya Ijumaa (5 Rajabu 1439h) sawa na (23 Machi 2018m), wamefanya nadwa kubwa ya kielimu na kuhudhuriwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Muhandisi Muhammad Ashiqar, na jopo la wasomi wa kisekula walio bobea katika mambo ya turathi za Iraq hususan turathi za mji mtukufu wa Karbala pamoja na wanafunzi wa vyuo vikuu, nadwa ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu, kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq wa jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi, halafu ukafuata wimbo wa taifa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kisha ukafuata ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu ulio wasilishwa na Ustadh Muhandisi Twalaal Biir, miongoni mwa aliyo sema ni: “Bila shaka mnajua umuhimu mkubwa wa turathi, kwani ndizo ambazo huwapa watu utambulisho wao na kuwatofautisha na wengine, pia huwapa heshima ya kijamii, kielimu na kimalezi, na ndio msingi wa tamaduni ambazo haziwezi kutengamaa kama sio juhudi za wasomi wa hauza na wa sekula za kutambulisha turathi hizo kwa umaa, jamba ambalo lilipotea kwa miongo mingi, hadi miaka ya hivi karibuni ndio limepata mtu wa kulisimamia naye si mwingine ni Mheshimiwa kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmadi Swafi, ambaye ameanzisha kituo cha turathi za Karbala na kutoa msaada kwa watafiti wa turathi katika mji wa Karbala, kwa kuzingatia kua turathi hazitengani na utamaduni wa mwanadamu, pia zina athari kubwa katika jamii na kutengeneza mustaqbali, pia huonisha yaliyo kuwepo wakati wa nyuma na sasa, vilevile husaidia kuendeleza jamii na kuifanya kua jamii bora katika sekta tofauti, juhudi za watendaji wote wa sekta hii ni kuhakikisha wanazitambulisha turathi za mji wa Karbala miongoni mwa vitabu na nyaraka zenye hazina kubwa ya elimu”.

Akasema: “Nadwa hii tukufu inayo fanywa kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Kufa ni sehemu ya kuthibitisha niliyo yasemwa, ya kujali na kuzipenda turathi za wanadamu, na kuchaguliwa kauli mbiu isemayo (Turathi za Karbala katika uchunguzi wa wana sekula) ni uthibitisho mwingine kua turathi zitatambulishwa kwa kukidhi vigezo vyote kwa kielimu baada ya kupasishwa na watu walio bobea katika utambuzi wa turathi za taifa letu tukufu”.

Akamaliza kwa kusema kua: “Nawaomba watu huru duniani kote wafuate nyayo zenu katika kuhifadhi turathi na kuzilinda, kwani kuzipoteza ni kupoteza utambulisho wao na utajo wao, nawaomba washiriki wote na kila aliye hudhuria hapa kufichua kadri mtakavyo weza mambo ya utafiti wa kielimu, pia naziomba taasisi na vikundi vya utafiti kuanzisha ushirikiano utakao shajihisha watafiti wa viwango vyote na kutoka kila sehemu wazitambulishe turathi za Karbala ambazo zina uwezo mkubwa wa kutengeneza mazingira ya jamii”.

Baada yake ukafuata ujumbe wa rais wa chuo kikuu cha Kufa ulio wasilishwa na Dokta Muhsin Abadi, ulio sema kua: “Tupo chini ya kivuli cha Atabatu Abbasiyya tukufu, ambayo ndio mlezi wa harakati hizi za kisekula, zilizo tanguliwa na mawasiliano ya mara kwa mara na juhudi za pamoja baina ya kituo cha turathi za Karbala na chuo kikuu cha Kufa, hii haikua kazi ya kwanza, hakika kituo cha turathi za Karbala kimesha fanya kazi nyingi kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Kufa, jambo linalo pelekea chuo kionekane kua ni kinara wa elimu na historia, na wakati huo huo kina nafasi kubwa katika mambo mbalimbali ya kielimu na kupitia wanachuoni wake kinatoa mchango mkubwa katika taasisi za kiraia”.

Kisha ukafunguliwa ukurasa wa darasa mjadala (nadwa) lililo ongozwa na Dokta Ali Haji pamoja na Dokta Falahu Rasuul Alhusseiniy, na zikawasilishwa tafiti sita, ambazo ni:

Utafiti wa kwanza: ulikua wa Dokta Zamaan Abedi kutoka katika chuo kikuu cha Karbala kitivo cha malezi na elimu za kibinadamu, usemao (Maandishi na waandishi wa Karbala hadi karne ya 13 hijiriyya).

Utafiti wa pili: ulikua wa Dokta Salmaan Haadi Aali Twa’amah, kutoka katika chuo cha kiislamu cha Lebanon, usemao (Turathi za mashairi ya Shekh Muhammad Taqi Twabari Alhaairiy, masomo na uhakiki).

Utafuli wa tatu: ulikua wa Dokta Murtadha Abdu Nabi Shawi, kutoka katika chuo kikuu cha Kufa kitivo cha Fiqhi, usemao (Shekh Abu Mahaasin Karbalai historia yake kwa ufupi na kuangalia ufasaha katika mashairi yake).

Utafiti wa nne: ulikua wa Dokta Hana Hussein Alwaan, kutoka chuo kikuu cha Kufa kitivo cha Fiqhi, usemao (Turathi za Haairiy katika kitabu cha Dhariah).

Utafiti wa tano: ulikua wa Dokta Ali Jafari Muhammad, kutoka katika chuo kikuu cha Kufa kitivo cha Fiqhi, usemao (Manhaji ya Shekh Abdu-Nabi Jazaairiy katika kitabu chake cha Jaawi Aqwaal).

Utafiti wa sita: ulikua wa Dokta Haajir Dawiir, kutoka katika chuo kikuu cha Kufa kitivo cha Malezi, usemao (Utafiti katika turathi za Shekh Muhammad Mahdi Naraqiy katika kitabu cha Jaamiu Afkaari wa Naaqidu Andhwaar namudhajiya).

Pia kulikua na baadhi ya maelezo na maswali yaliyo elekezwa kwa watoa mada kutoka kwa wasikilizaji, nao walijibu na kutoa ufafanuzi pale ulipo hitajika, fahamu kua katika nadwa hii kulikua na tafiti (24) kutoka vyuo vikuu tofauti vya hapa Iraq, mwisho wa nadwa watafiti walio shiriki kutoa mada walitunukiwa midani na vyeti vya ushiriki.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: