Maandalizi ya ufunguzi wake: Mafundi na wahandisi wa kituo cha kibiashara cha Afaaf wanafanya matengenezo ya mwisho…

Moja ya kumbi za kituo cha kibiashara
Kituo cha kibiashara cha Afaaf kipo katika hatua za mwisho za ujenzi, kwa ajili ya ufunguzi katika siku chache zijazo, huu ni moja ya miradi muhimu ya kiuchumi inayo endeshwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, unao lenga kutoa huduma za kibiashara kwa wakazi wa Karbala na watu wote wanao kuja Karbala, sehemu hiyo zitapatikana bidhaa zinazo tengenezwa ndani ya nchi na za kigeni kwa bei nafuu itakayo msaidia mlaji.

Muhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu, ametuhadithia kazi muhimu zinazo endelea hivi sasa, amesema kua: “Kituo cha kibiashara kipo katika hatua za mwisho, tayali mambo mbalimbali yamesha kamilika kama vile (Umeme, (AC), zima moto, kamera, alam za tahadhari, intanet na vinginevyo), hali kadhalika ufungaji wa lifti za mizigo na za watu umesha kamilika, na sehemu zote zimesha safishwa, tayali yumesha pokea kazi ya kwanza kutoka kwa shirika linalo tekeleza mradi huu (shirika la ujenzi la ardhi tukufu) tunasubiri kakamilika baadhi ya mambo ya mwisho kisha tukabidhiwe rasmi na kufanya ufunguzi wa jengo hili la kibiashara”.

Akaongeza kusema kua: “Wataalamu wa shirika linalo tekeleza mradi huu wametumia uwezo wao wote kuhakikisha wanafanya kazi hii kwa ubora wa hali ya juu na ndani ya muda ulio pangwa, na kitengo cha miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu kiliwapa kila aina ya ushirikiano kwa ajili ya kuwarahisishia utendaji wa kazi, na kuharakisha kazi, jambo lililo saidia kumaliza kazi kwa wakati tena kwa kufuata utaratibu ulio wekwa”.

Kumbuka kua kituo cha kibiashara cha Afaaf kwa mujibu wa maelezo ya Muhandisi Dhiyaau Swaaigh: “Kitakua kituo cha mfano cha kibiashara katika mkoa mtukufu wa Karbala, kwa sababu kimeplaniwa kisasa zaidi, na kitachangia kukuza soko la biashara, kitatoa huduma kwa wakazi wa Karbala na kila aneye kuja katika mji huu, pia kitakua na umakini mkubwa wa kukagua bidhaa zake na kuhakikisha hakuna bidhaa feki au zisizo faa zitakazo uzwa katika jengo hili kwa ajili ya kuwalinda walaji”.

Fahamu kua mradi huu umejengwa katika mtaa wa Hussein (a.s) ndani ya mkoa wa Karbala katika eneo lenye ukubwa wa (2m2600), na lina ghorofa tatu, zenye sehemu kuu mbili: sehemu ya biashara (soko) na sehemu nyingine ya ofisi mbalimbali na magodauni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: