Jibu kwa yaliyo andikwa katika mitandao ya kijamii: Shirika la Nurul-Kafeel latoa maelezo kuhusu uwepo wa kuku za Alkafeel zisizo faa kwa matumizi ya binadamu…

Maoni katika picha
Mitandao ya kijamii hivi karibuni imeandika kua uongozi wa afya wa mkoa mtukufu wa Karbala umebaini kuwepo wa kuku za Alkafeel zisizo faa kwa matumizi ya binadamu, jibu la madai hayo ambayo hayana ukweli wowote, Shirika la Nurul-Kafeel limetoa maelezo yafuatayo:

Kwa raia wote watukufu na wadau wetu weto..

Hakika yaliyo andikwa katika mitandao ya kijamii hivi karibuni, madai kua uongozi wa afya wa mkoa wa Karbala kitengo cha usimamizi wa afya kimekiri kuwepo kwa zaidi ya tani (9) za kuku za Alkafeel zisizo faa kwa matumizi ya binadamu.

Tunapenda kutoa maelezo yafuatayo:-

  • Duka linalo daiwa kukutwa na kuku za Alkafeel lipo katika sehemu ya kibiashara katika mkoa mtukufu wa Karbala, halina uhusiano wowote na shirika la Nurul-Kafeel, sio wakala wa shirika wala sio miongoni mwa vituo vya mauzo ya moja kwa moja vya shirika.
  • Hakika shehena ya kuku walizo kutwa nazo, iliuziwa duka hilo katika kipindi cha ziara ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) iliyo pita nyaraka rasmi za mauzo zinathibitisha hilo.
  • Hakika duka tajwa ndio wanao wajibika kwa kutoziuza kuku hizo kwa wakati muafaka na kwa utunzaji mbaya ulio pelekea zikaharibika, fahamuni kua waranti wa mzalishaji ulikua unaisha mwezi wa kumi (2018) hakika shirika halihusiki na jambo hilo.
  • Wamiliki wa duka hilo walilitembelea shirika siku ya Alkhamisi ya (22/03/2018m) wakaomba radhi kwa yaliyo tokea na wakaahidi kuwajibika kutokana na mapungufu yao katika utunzaji.
  • Hakika tangu kuanzishwa kwa Shirika la Nurul-Kafeel hadi leo limekua makini sana na hufanya uchunguzi wa kina katika bidhaa zake zote kabla ya kuziingiza katika soko la Iraq, huangalia waranti wa kiwanda na mwisho wa matumizi, na bidhaa zetu zitokazo nje ya nchi hufanyiwa vipimo vyote katika maeneo ya mipakani, tuna vielelezo vya kila kitu kwa mujibu wa kanuni za afya, wala hua hatupokea bidhaa yeyote ambayo haijatimiza masharti, kuna bidhaa ambazo hazikutimiza masharti shirika lilizikataa kabla ya kuziingiza hapa nchini kwa ajili ya kulinda afya za wananchi.
  • Tunawapongeza watumishi wa idara ya afya ya mkoa mtukufu wa Karbala kwa kazi nzuri wanayo fanya ya kuchunguza na kufatilia ubora wa bidhaa zinazo zalishwa na viwanda vyote kwa ajili ya kulinda afya za raia wake.
  • Tunawaomba raia wote watukufu washirikiane na Shirika wakati wowote watakapo baini tatizo lolote kwenye bidhaa zetu, ili Shirika lifanye haraka kuondoa tatizo hilo, mnaweza kupiga simu kwa kutumia moja ya namba zifuatazo:-

07801966622

07801966624

07817394401

Au unaweza kutuandikia kupitia barua pepe hii:- hq@islamicalkafeel.com.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: