Kamati ya majaji wa shindano la (Milango ya rehma) la picha cha mnato (photography) yatangaza majina ya washindi…

Maoni katika picha
Kamati ya majaji wa shindano la (Milango ya rehma) la picha za mnato (photography) lililo endeshwa na kitengo cha miradi ya kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza majina ya washindi kumi, na wamesisitiza kua kazi zao zilikua na ubora wa hali ya juu, zimekidhi vigezo vyote vya kitaifa na kimataifa, pia zimekidhi matakwa ya shindano hili kuhusu milango ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na zinazingatiwa kua miongoni mwa kazi bora za kiutaalamu zilizo fanywa na mikono ya raia wa Iraq.

Majina ya walio faulu kwa mpangilio wa ufaulu wao kuanzia wa kwanza hadi wa kumi:

  • 1- Ihaabu Mundhir kutoka mkoa wa Diwaniyya.
  • 2- Dhiyaau Azizi kutoka mkoa wa Karbala.
  • 3- Muhammad Ali Hassan kutoka mkoa wa Karbala.
  • 4- Sajaad Hassan kutoka mkoa wa Baabil.
  • 5- Israa Miqdad kutoka mkoa wa Karbala.
  • 6- Twaiba Haatam kutoka mkoa wa Karbala.
  • 7- Sajaad Abdu-Zuhra kutoka mkoa wa Karbala.
  • 8- Ali Murtadha Hussein kutoka mkoa wa Karbala.
  • 9- Dhiyaau Shaakir Karim kutoka mkoa wa Karbala.
  • 10- Muhammad Adhim kutoka mkoa wa Karbala.

Kamati ikasema kua hafla ya kugawa zawadi kwa washindi hao itafanyika katika ukumbi wa Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kumbuka kua kamati umeandaa zawadi zifuatazo kwa washindi:

Mshindi wa kwanza: (1,000,000) milioni dinari za Iraq.

Mshindi wa pili: (500,000) laki tano dinari za Iraq.

Mshindi wa tatu: (250,000) laki mbili na elfu hamsini dinari za Iraq.

Mshindi wa nne hadi wa kumi: (150,000) laki moja na elfu hamsini dinari za Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: