Kamati ya wahariri wa jarida la Baahir yatangaza kupokea tafiti za kielimu kwa lugha ya kiengereza tu…

Maoni katika picha
Kamati ya wahariri wa jarida la Baahir imetangaza kupokea tafiti za kielimu, katika sekta ya elimu za mazingira na uhandisi kwa lugha ya kiengereza tu, na inaomba radhi kwa kutopokea tafiti zilizo andikwa kwa lugha ya kiarabu, inawaomba watafiti kutuma tafiti zao za kielimu zilizo kidhi vigezo vya kielimu vinavyo julikana kimataifa, utafiti usiwe umesha wahi kutolewa siku za nyuma na haujawahi kutangazwa na chombo chochote, kamati imebainisha kua: tafiti zote zitumwe kupitia toghuti ya jarida: albahir.alKafeel.net au barua pepe ifuatayo albahir@alameedcenter.iq kwa kujaza fomu na kuituma kupitia program ya (Word) na aina ya hati iwe (Times New Roman), ukubwa wa maandishi katika vichwa vya mada kuu uwe saizi (16) na vichwa vya mada ndogo uwe saizi (14), utafiti wote uandikwe kwa herufi za saizi (14), ukurasa wa kwanza uandikwe, jina la utafini, jina la mtafiti, sehemu ya kazi, namba ya simu na anuani ya barua pepe.

Kumbuka kua jarida ya Baahir ni jarida la kielimu linalo tolewa na kituo cha (Ameed duwaliyyu lilbuhuthi wa dirasaat), chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, ambapo hutolewa mara mbili kwa mwaka, na kila toleo hua na vitu vingi, pia linatambuliwa na wizara ya elimu ya juu na utafiti wa kielimu hapa Iraq, linategemewa kwa mchango wake katika elimu, lipo chini ya kanuni ya (IASJ).

Kwa maelezo zaidi kuhusu jarida hili, unaweza kuangalia mtandao ufuatao: https://albahir.alkafeel.net/rules/
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: