Rais wa kamati ya matangazo ya kongamano la kimataifa na kitamaduni Rabiu Shahada awamu ya kumi na nne na msaidizi wa kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Aqiil Abdulhussein Yasiri ametangaza ratiba kamili ya kongamano litakalo anza tarehe tatu Shabani (1439h) hadi tarehe saba ya mwezi huo, chini ya usimamizi wa uongozi mkuu wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kwa ajili ya kuhuisha nuru za Muhammadiyya (a.s), likiwa na kauli mbiu isemayo: (Kwa utukufu wa Hussein (a.s) tumepigana na kwa utukufu wa fatwa tumeshinda).
Akasisitiza kua awamu hii itakamilisha mazuri ya awamu zilizo tangulia, awamu hii itakua na mazingira maalum kwa sababu ndio mwaka wa kwanza ambao linafanyika kongamano baada ya kukombolewa kwa ardhi yote ya Iraq kutoka katika udhibiti wa magaidi wa Daesh.
Kuhusu ratiba amebainisha kua imeandaliwa na kamati ya maandalizi ya kongamano, ambapo inaonyesha yatakayo fanyika katika siku zote tano za kongamano na tayali imesha chapishwa kwa lugha mbili ya Kiarabu na Kiengereza kama inavyo onekana.