Kufuatia mfululizo wa nadwa zinazo lenga kukuza kilimo: Shirika la Aljuud linafanya nadwa ya kutambulisha bidhaa zake na faida zake katika kuongeza mavuno…

Sehemu ya nadwa
Shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Aljuud lililo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, bado linaendelea na kufanya nadwa za kutambulisha bidhaa zake kwa wakulima katika mikoa tofauti ya Iraq, kwa kufuata ratiba maalum, kwa ajili ya kuboresha kilimo kwa kufuata njia za kisasa kuanzia wakati wa kuandaa shamba hadi wakati wa mavuno, shirika limesha pata mafanikio katika maeneo mengi ambako walifuata utaratibu wa kilimo cha kisasa na wakafanikiwa kuongeza mavuno yao.

Nadwa hii ya sasa inafanyika katika mkoa wa Karbala, nadwa hii imepewa jina lisemalo: (Utalamu wa kilimo ni mlango unao elekea kukuza sekta ya kilimo), kwa kushirikiana na ofisi ya utafiti na upasishaji wa mbegu, ndani ya ukumbi wa kituo cha utafiti, na kuhudhuriwa na wakulima wakubwa pamoja na wadau wa kilimo, bidhaa za shirika zina mafanikio makubwa katika kuongeza mavuno wakiwa na usemi wa mashuke ya dhahabu.

Muhandisi Imaad Ali Bahadeli ambaye ni mkuu wa kiwanda cha mbolea cha shirika la Aljuud alikuwepo katika nadwa hii na alikua na haya ya kusema: “Lengo la kufanya nadwa hizi ni kuzitambulisha bidhaa za shirika la Aljuud na ufanyaji kazi wake kwa wakulima, katika nadwa hii tunaelezea baadhi ya bidhaa zinazo saidia kwa kiasi kikubwa kuongeza uzalishaji wa mazao hasa zao la ngano, shirika halita kua bahili wa kufikisha taarifa na elimu kwa wakulima ili waweze kuongeza uzalishaji wao kwa kutumia teknolojia za kisasa katika sekta ya kilimo, katika mazingira ambayo Iraq inapitia kwa sasa ya upungufu wa maji na uchache wa aridhi yenye rutuba”.

Muhandisi wa kilimo bwana Haidari Abdu Zuhra mkuu wa ofisi ya utafiti na upasishaji wa mbegu katika mkoa mtukufu wa Karbala amesema kua: “Bidhaa za shirika la Aljuudi zimesha tumiwa katika mikoa tofauti ya Iraq, na zimefanyiwa majaribio mbalimbali na yote yametoa mafanikio makubwa, haya ndiyo tunayo shuhudia katika badhaa za shirika hili”.

Nadwa ilipambwa na maoni mbalimbali pamoja na maswali mengi, yalitolewa majibu na ufafanuzi wa yale yaliyo hitaji kufafanuliwa, mwisho wa nadwa hiyo washiriki walitembelea moja ya shamba lililo tumia mbolea na bidhaa zinazo tengenezwa na Shirika hili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: