Kwa ajili ya kuangalia mafanikio na uzowefu wake: Atabatu Abbasiyya tukufu inakusudia kufanya maonyesho ya miradi yake…

Maoni katika picha
Kufuatia ufunguzi wa kituo cha kibiashara cha Afaaf, kinacho tarajiwa kufunguliwa siku chache zijazo, na kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Ali bu Abu Twalib (a.s), Atabatu Abbasiyya tukufu inakusudia kufanya maonyesho ya miradi yake ya (elimu, ujenzi, afya, malezi na masomo, kilimo, biashara, uchumi, utalii na viwanda) kwa mujibu wa maelezo ya mjumbe wa kamati inayo simamia maonyesho hayo Ustadhi Muhammad Aali Taajir.

Alisema kua: “Fikra ya kufanya maonyesho makubwa katika uwanja wa kituo cha kibiashara cha Afaaf imekuja hivi karibuni, baada ya kukubaliwa na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, imeundwa kamati ya kusimamia maonyesho hayo, yatakayo fanywa kwa mara ya kwanza na Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya kauli mbiu isemayo (Miradi yetu inashajihisha uwezo wa taifa) kuanzia tarehe (13 Rajabu 1439h, sawa na 29 Machi 2018m) na yataendelea kwa muda wa siku kadhaa asubuhi na jioni, kwa ajili ya kuwaonyesha wana nchi na mazuwaru pamoja na taasisi za kiserikali na zinginezo harakati na kazi zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu na huduma inazo toa, kwa upande mwingine kuonyesha mafanikio waliyo fikiwa katika sekta mbalimbali yanayo endana na maendelea ya dunia”.

Taajir akabainisha kua: “Watakao shiriki katika maonyesho haya ni: (Shirika la usalama Alkafeel, kitengo cha mgahawa pamoja na kitengo cha nidham, shirika kuu la uchumi likihusisha shirika la Aljuud, shirika la maji Alkafeel pamoja na vitengo vingine vya mashirika, shirika la bendera ya kimataifa, kitengo cha miradi ya kihandisi, kitengo cha zawadi na nadhiri, kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu, kitengo cha habari na utamaduni kikihusisha Maahadi ya Alkafeel ya kuongeza elimu na kukuza vipaji, idara ya intanet, kituo cha uchapishaji cha Alkafeel, kitengo cha makumbusho cha Alkafeel, Darul-Kafeel ya uchapishaji na usambazaji, idara ya kunufaika na mitambo, shirika la Nurul-Kafeel, hospitali ya Alkafeel, kitengo cha utumishi, uongozi wa kituo cha Afaaf, kiwanda cha Ataba tukufu cha kutengeneza milango na madirisha ya makaburi, chuo kikuu cha Ameed, mradi wa kijana mzalendo wa Alkafeel) hii ni sehemu ndogo ya harakati za Ataba tukufu, kama tukifungua milango kwa vitengo vyote maonyesho yatakua makubwa sana na nafasi itakua ndogo”.

Akasisitiza kua: “Vile vile kutakua na mashirika ya kimataifa yanayo jihusisha na mambo mbalimbali yatakayo shiriki katika maonyesho hayao, yatakayo endelea kwa muda wa siku kadhaa, tunatoa wito kwa watu wote wa ndani na nje ya mkoa wa Karbala waje kuangalia maonyesho haya na kutambua shuguli zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: