Tangu kuanzishwa kwa chuo kikuu cha Ameed kilicho chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kiliweka sera ya kuwatumia wasomi wa kiiraq waishio nchini na nje ya nchi, na kunufaika na utaalamu wao kwa ajili ya kuendeleza taaluma.
Hivi karibuni chuo kimemwalika daktari wa kiiraq aishie ughaibuni Dokta Jafari Kaarim, daktari bingwa wa maradhi ya fizi na mkufunzi wa chuo kikuu cha Toronto Kanada, Mkuu wa kitivo cha udaktari wa meno Dokta Baasim Zuwain alimtembeza mgeni wake sehemu mbalimbali za chuo, na katika kitivo cha udaktari wa meno, akamuonyesha selibasi za masomo pamoja na kumbi za madarasa, kisha mgeni alitoa muhadhara kuhusu mambo mawili muhimu katika sekta ya udaktari wa meno na maradhi ya fizi.
Alitoa muhadhara ndani ya ukumbi mkuu wa chuo na kuhudhuriwa na rais wa chuo kikuu pamoja na jopo la wakufunzi na wanafunzi wa chuo, katika muhadhara wake alizungumzia mafanikio ya kisasa zaidi katika fani hii na vifaa tiba vinavyo tumika.
Miongoni mwa mambo aliyo tuambia Dokta Jafari Kaarim ni: “Nina furaha kubwa sana kwa kuwepo katika uwanja huu wa elimu kubwa ambao natarajia utakua na mustaqbali mwema, mada yangu inalenga kuelezea misingi ya kazi ya kutibu meno na namna ya kutumia misingi hiyo, pamoja na namna ya kutibu fizi zilizo haribika kutokana na matibabu ya meno, na kufafanua matatizo yanayo weza kutokea katika fizi unapo tumia njia za upasuaji za kisasa, nimeelezea njia mbalimbali zinazo weza kutumika katika kutibu fizi zilizo haribika kutokana na matibabu ya meno, ambapo kuna matibabu ya kutumia dawa tu, na matibabu ya njia ya upasuaji”.
Kumbuka kua chuo kikuu cha Ameed ni moja ya taasisi za kielimu zilizo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, na kimefungua kitivo kwa kwanza cha udaktari chenye kiwango sawa na vyuo binafsi vya udaktari, na wanafuata selibasi ya kimataifa, kwa ajili ya kuboresha uwezo wake na kufikia kiwango cha kimataifa hualika wataalamu bingwa wenye uzowefu mkubwa kila baada ya muda fulani na kunufaika na uzowefu wao na kuutumia katika njia sahihi ili chuo hiki kiweze kuchuana na taasisi za kielimu za kimataifa.