Maahadi ya Qur’an tukufu yamtunuku Ijaza ya kisomo cha riwaya ya Hafsa kutoka Aaswim mmoja wa wasomaji wa kiiran…

Maoni katika picha
Miongoni mwa harakati mbalimbali za Qur’an zinazo endelea, Maahadi ya Qur’an tukufu ya Atabatu Abbasiyya imemtuniku Ijaza ya usomamji wa kisomo cha riwaya ya Hafsa kutoka Aaswim mkuu wa redio ya Qur’an tukufu ya Iran, msomaji maarufu wa Qur’an bwana Ahmadi Abu Qassimiy, baada ya kupewa mtihani wa kusoma Qur’an na kuhojiwa hadharani katika ukumbi wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) chini ya kamati ya wasomi iliyo undwa na wajumbe wafuatao, Shekh Farasi Twaaiy, Sayyid Haidari Haidariy na Dokta Husaam Juburiy, na ushiriki wa viongozi wa Atabatu Abbasiyya mlezi wa tukio hili, ulio wakilishwa na katibu mkuu wa Ataba tukufu, Muhandisi Sayyid Muhammad Ashiqar na mkuu wa Maahadi ya Qur’an tukufu Shekh Jawaad Naswirawi na mkuu wa kituo cha miradi ya Qur’an Sayyid Hussein Halo.

Kwa mujibu wa watalamu wa fani za Qur’an, tukio hili ni muhimu sana na msingi mzuri kwa mustaqbali, litasaidia kuitangaza Maahadi na kuifanya iwe inashiriki katika matukio mbalimbali yanayo husu Qur’an.

Bwana Farasi Twaaiy amebainisha kua: “Hakika hili ni miongoni mwa matukio muhimu kimataifa, ndani ya uwanja wa Abulfadhil Abbasi (a.s) tunatuma wito kwa wasomaji wote wa Qur’an tukufu, waongeze juhudi ya kua na kisomo kizuri ili waweze kupata Ijaza hii, jambo hili tumelirithi kutoka kwa watangulizi wetu wema, miongoni mwao ni Allamah Dokta Hussein Ali Mahfudh (r.a), hatua hii ni nzuri na tunatarajia zifuate hatua zingine katika kuitumikia Qur’an tukufu”.

Naye Abu Qassimiy ameishukuru Atabatu Abbasiyya tukufu na Maahadi ya Qur’an pamoja na kituo cha miradi ya Qur’an kwa kukubali ombi lake na kusimamia Ijaza hii yenye umuhimu mkubwa kwake.

Sambamba na tukio hilo, imefanyika mahafali ya Qur’an tukufu chini ya mradi wa (Arshi Tilawah) iliyo somwa na Liith Abidiy, mmoja wa wanafunzi wa mradi wa kitaifa wa kuandaa wasomi wa kiiraq, ikafuata kaswida iliyo imbwa na Ustadh Muhammad Ali Dahashti, mkuu wa kikosi cha Alghadiir cha usomaji wa Qur’an na kaswida za kiislamu nchini Iran, halafu ikafuata Qur’an iliyo somwa na Ustadh Ahmadi Abu Qassimiy, mkuu wa redio ya Qur’an tukufu ya Iran.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: