Kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi akagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa floo ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) unao endelea hivi sasa, alisikiliza maelezo kutoka kwa rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi, Muhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh na kitengo cha uangalizi wa kihandisi, Muhandisi Abbasi Mussa Ahmadi, kwani wao ndio wasimamizi wakuu wa utekelezaji wa mradi huu, unao husisha ujenzi wa floo ya haram tukufu na uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), walielezea hatua waliyo fika katika ujenzi na hatua zijazo, pamoja na mambo ya kitalamu na kihandisi wanayo tumia katika kujenga floo hiyo, kuanzia utoaji wa marumaru za zamani hadi hatua ya kuweka marumaru za sasa na kukarabati maeneo yenye matatizo.
Sayyid Swafi amesisitiza kuongeza juhudi na kuhakikisha kazi inakamilika kwa muda ulio pangwa na kwa ubora mkubwa, na akasifu kazi nzuri iliyo fanyika katika hatua zilizo pita.
Muhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi cha Atabatu Abbasiyya tukufu amebainisha kua: “Kazi inaendelea kama ilivyo pangwa na kwa kufuata mgawanyo ulio fanywa katika haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na inaendelea kwa kasi, watendaji wa mradi huu wanafanya kila wawezalo kwa ajili ya kukamilisha mradi huu kwa muda ulio pangwa”.
Kumbuka kua haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imeshuhudia utekelezwaji wa miradi mbalimbali, iliyo tekelezwa kwa muda maalumu kutokana na umuhimu wa kila mradi, kama vile mradi wa upanuzi wa haram, ujenzi wa paa la haram, pamoja na kufunika kuta za Ataba tukufu, ujenzi wa sardabu (tabaka la chini ya usawa wa ardhi) uliu fanyika katika haram tukufu, pamoja na kutengeneza na kuweka dirisha tukufu na sistim zingine, kama vile sistim ya (AC), zima moto, utoaji wa tahadhari, mawasiliano, ulinzi na miradi mingine mingi ambayo nafasi haitosi kueleza yote, orodha ndefu ya miradi iliyo fanyika inakamilishwa na mradi huu wenye umuhimu sawa na iliyo tangulia ambao ni mradi wa kujenga floo ya haram tukufu kwa kutoa marumaru za zamani zilizo wekwa tangu miaka ya sabini ya karne iliyo pita na kuweka marumaru mpya.