Miongoni mwa matembezi yao yanayo lenga kuwajenga wafuasi wa Ahlulbait (a.s) katika miji na vitongoji vya Kashmiri, ugeni wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya umetembelea kitongoji cha (Majhuisidaan) katika mji wa Kashmiri nchini Pakistan, ugeni huo ulipokelewa na idadi kubwa ya wanachuoni wa kisunni wa mji huo na wengine waliokuja kutoka miji mingine kwa ajili ya kukutana na ugeni huo.
Walifanya mazungumzo ya kidini yaliyo ongozwa na kiongozi wa wageni kutoka katika Ataba mbili tukufu Sayyid Adnaan Jalukhaan Mussawi, ujumbe wa wanachuoni wa kisunni walielezea utukufu wa kiongozi wa waumini (a.s), naye Sayyid Jalukhaan akaelezea mambo wanayo kubaliana vitabu vya pande mbili.
Sayyid Jalukhaan akabainisha kua: “Sijashangazwa na maneno ya ujumbe wa wanachuoni wa kisunni wenye mlengo wa sufi, hakika wao wanaamini utukufu wote wa kiongozi wa waumini (a.s) na kua alikua na haki zaidi kushinda maswahaba wote, na alikua mtu wa karibu zaidi kwa Mtume (s.a.w.w) bila ubishi”.
Akaongeza kua: “wamesisitiza mara nyingi kua (Ali yupo pamoja na haki na haki ipo pamoja na Ali) na kwamba yeye (a.s) ni mtu muhimu katika thikri zao na wanajikurubisha kwa Mwenyezi Mungu mtukufu kwa kumpenda, na wanaamini kua anaukaribu wa pekee kwa Mwenyezi Mungu”.
Wanachuoni wawili waliomba ruhusa ya kusoma kaswida inayo elezea mapenzi ya kiongozi wa waumini na ulazima wa kumtii baada ya Mtume (s.a.w.w).
Kwa upande mwingine ujumbe huo ulikutana na Allamah Sayyid Muhammad Ali Halo, mwakilishi wa ugeni wa Atabatu Husseiniyya tukufu na wakamhakikishia kua “Wanahamu kubwa ya kuona jina la kiongozi wa waumini (a.s) limeandikwa katika kila sehemu ya dunia”, naye Allamah “Halo” akawaambia: jambo hilo ndio alilo kua akilitaka Mtume (s.a.w.w).
Baada ya hapo walishiriki katika zowezi la kupandisha bendera ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kitongoji hicho na wakazi wa mji huo waliona kua huo ni utukufu mkubwa sana kwao.
Kumbuka kua kitongoji cha Majhuisaidaan kilichopo katika mji wa Kashmiri ni miongoni mwa vitongoji kongwe katika kuukubali ushia, ziara hii ni miongoni mwa ziara zinazo fanywa baada ya kumaliza kongamano la kitamaduni msimu wa Karbala (Nasimu Barbala) katika nchi ya Pakistani linalo simamiwa na Atabatu Husseiniyya tukufu na hushiriki Atabatu Abbasiyya tukufu.