Bendera ya Abulfadhil Abbasi inapepea katika mji wa Kashmiri Pakistan.

Maoni katika picha
Wapenzi wa Ahlulbait (a.s) walimiminika kwa wingi kuupokea ugeni kutoka katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya walio kwenda katika mji wa Madhfar-Abaad mji mkuu wa Kashmiri, tangu mara ya kwanza ya kuwasiri kwa ugeni huo katika ardhi ya mji huo, wenyeji wa mji huo walimiminika kuwapokea, pia walipata mapokezi rasmi kutoka kwa uongozi wa mji huo, na kulikua na sherehe kubwa ya kupokea bendera za Abu Abdillahi Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), zilizo pandishwa katika anga la mji huo, uliopo kaskazini magharibi ya Pakistan ukipakana na India na China, sherehe zilizo fanywa katika mji wa (Majhuisaidaan) katika malalo ya mmoja wa wajukuu wa Imamu Swadiq (a.s), ambaye ni maarufu kwa jina la Shaha Bokhari aliye pandisha bendera ya Imamu Hussein (a.s) kwa mara ya kwanza katika mji huo kabla ya miaka 400.

Sherehe hizo zilifunguliwa kwa Qur’an iliyo somwa na Muadhini wa Ataba mbili tukufu bwana Aadil Karbalai, kisha ukafuata ujumbe ulio wasilishwa na Sayyid Adnaan Jalukhaan Imamu wa jamaa katika ukumbi mtukufu wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ambaye alibainisha kua:

Enyi mabwana na mabibi enyi wakazi wa mji huu mtukufu, naono kundi kubwa la watu mlio kusanyika chini ya hema la Imamu Hussein (a.s), huku tukikumbuka usemi usemao (kila ardhi ni Karbala na kila siku ni Ashura), yatupasa kumshukuru sana Mwenyezi Mungu, sisi tunaishi karibu na malalo mawili matukufu, baada ya kuona mapenzi yenu kwa bwana wa mashahidi, jambo hilo linatuwajibisha kufikisha ujumbe wa Imamu Hussein kwa wafuasi wake duniani, na ndio maana tumekuja hapa tukiwa na bendera ya Bwana wa Mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), tunamuomba Mwenyezi Mungu awawezesheni kutembelea malalo ya maimamu wenu watukufu, hakika nyie mnastahiki zaidi jambo hilo kutokana na mapenzi makubwa mliyo nayo kwao.

Baada ya hapo wageni pamoja na wenyeji wa mji huo wakaelekea katika shughuli ya kupandisha bendera tukufu.

Katika shughuli hiyo uongozi wa wakfu wa mambo ya dini wa mji wa Kashmiri Pakistan ulifanya kongamano lililo hudhuriwa na wageni kutoka katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, kongamano ambalo lilihitimisha shughuli za kongamano la msimu wa Karbala awamu ya tano katika mji mkuu wa Islamabad, aidha kongamano hilo lilihudhuriwa na wawakilishi wa dini na tabaka tofauti za wakazi wa mji huo, lilifunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha ukafuata ujumbe ulio tolewa na Shekh Nadhir Hassan Kilani mkuu wa wakfu wa dini ambaye alisema kua:

Tunawakaribisha sana ndugu zetu wageni kutoka katika Ataba mbili tukufu, tumepata utukufu mkubwa sana kwa kufikiwa na ugeni huu katika mji wetu, ziara yanu hii ni dalili ya wazi kua mnajali mambo ya waislamu, tunapenda kuwajulisha kua katika kongamano hili tunao washiriki kutoka katika dini na madhehebu tofauti wakionyesha umoja na mshikamano pamoja na ndugu zao waislamu bila kujali dini wala madhehebu.

Akafafanua kua: Katika mji huu tulipata mtihani wa makundi yaliyo taka kuingiza fitna ya ubaguzi kutoka kwa maadui walewale wanao eneza ubaguzi na ugaidi katika miji mingi ya waislamu, wanatumia kuwashawishi waislamu wenye imani dhaifu, lakini tumesimama pamoja kupambana na watu hao na kuharibu njama zao, tumeongeza umoja na mshikamano na kuuzuia ugonjwa huo usiingie ndani ya jamii yetu, tumesikia na tumeona yaliyo fanywa na Marjaa dini mkuu wa Iraq katika kupambana na ubaguzi, na namna anavyo unganisha raia wa Iraq katika mapambano dhidi ya magaidi wa Daesh, kwa hakika ni fahari kubwa kwa waislamu kwa kupatikana Marjaa mwema kama huyu, tunawashukuru sana, nakuambieni tena karibuni katika mji wenu wa pili na kwa ndugu zenu wapenzi.

Halafu ukafuata ujumbe wa Ataba mbili tukufu ulio wasilishwa na Sayyid Adnaan Jalukhaan Mussawi ambaye alisema kua:

Inatufurahisha sana kusimama mbele ya ndugu zetu watukufu katika kongamano hili, huku tukijikumbusha aliyo kuja nayo Mtume (s.a.w.w) miongoni mwa misingi ya ujumbe wake ni kuunganisha watu na kuhakikisha waislamu wanasimama mstari mmoja na wanashikamana katika kamba ya Mwenyezi Mungu na wala hawafarakani, hakika hiyo ndio njia ya uongofu wa umma, pia alitubainishia kua uislamu ni dini ya maelewano, dini ya undugu na kuishi kwa mapenzi, ni lazima kwa mwislamu amlinde ndugu yake mwislamu katika mali na heshima yake, na huu ndio mwenendo wa Ahlulbait (a.s), walikua wanalingania upendo baina ya watu na kulinda heshima ya mwanadamu kama ilivyo kuja ndani ya Qur’an tukufu, kuhusu umuhimu wa kulinda heshima ya mwanadamu, na kuto wadharau watu au maisha ya watu, kama tunavyo shuhudia leo vitendo vinavyo fanywa na vikundi vya watu walio potea na kutumia jina la kiislamu wakati hawana hata chembe ya uislamu, wanaua na kudhalilisha watu kwa kutumia jina la dini wakati wako mbali kabisa na mafundisho ya dini, tunamuomba Mwenyezi Mungu awaunganishe waislamu wa mashariki na magharibi na ailinde miji yao hakika yeye ni msikivu na mjuzi.

Kisha ukafuata ujumbe wa Mheshimiwa Sayyid Muhammad Ali Halo kutoka katika hauza ya NaJafu Ashrafu ambaye alisema kua:

Inatufurahisha kusimama pamoja na wanachuoni watukufu wa mji huu, huku tukishuhudia juhudi zao za kuhakikisha wanaishi kwa amani na watu wa tabaka tofauti katika mji wao, hili ni jambo la kufurahisha, wala tusisahau uzowefu wa Maimamu wa Ahlulbait (a.s) namna walivyo ishi na wanachuoni wa madhehebu zingine, Maliki bun Anasi alikua anakwenda kusoma kwa Imamu Jafari Swadiq (a.s) na Imamu Jafari alikua anampa umuhimu mkubwa, pia tukumbuke maneno ya maimamu wa madhehebu wanazungumza vipi kuhusu Ahlulbait (a.s), miongoni mwao ni Muhammad bun Abu Miqdadi anasema: (Sikuwahi kuingia kwa Jafari ispokua nilimkuta anaswali au anafanya dhikri au kasimama), hali kadhalika Ahmadi bun Hambali ambaye ameelezea sana utukufu wa Ahlulbait (a.s), bila kumsahau Imamu Shafi ambaye vitabu vyake vimejaa utukufu wao.

Akafafanua kua: Hakika uzowefu wa kuishi kwa amani unao zungumzwa na wanachuoni wetu hatuwezi kuufumbia macho, hususan katika kipindi cha hivi karibuni baada ya kuingia magaidi wa Daesh na kujaribu kuleta fitna ya ubaguzi, walijibiwa na sauti ya Marjaa pamoja na umma wa vijana wa miji ya kusini na ya kati, walio miminika kwenda kuwanusuru ndugu zao katika miji ya magharibi, wakapigana kishujaa hadi wakaikomboa miji hiyo, tunamuomba Mwenyezi Mungu awalinde waislamu wote na awaunganishe wawe kitu kimoja hakika yeye ni msikivu na mjibuji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: