Usiku wa kuzaliwa mlango mkusudiwa Imamu Muhammad Jawaad (a.s)…

Maoni katika picha
Umma wa kiislamu na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) duniani kote katika usiku wa mwezi kumi Rajabu wanakumbuka kuzaliwa kwa nuru ya Tisa miongoni mwa nuru za Maimamu, naye ni Imamu Muhammad Jawaad (a.s), aliye julikana kwa elimu yake, na akatoa mchango mkubwa sana katika madrasa ya Ahlulbait (a.s) na kuhifadhi turathi zao kwa kufundisha wanachuoni na wanafunzi njia (selebasi) za kujifundisha sheria za kiislamu.

Imamu Jawaad, ni Muhammad bun Ali bun Mussa bun Jafari bun Muhammad bun Ali bun Hussein bun Ali bun Abu Twalib (a.s), mama yake ni bibi Sakina Marsiyya na inasemekana ni Khizaraan, mke wake alikua anaitwa bibi Sumana mmorocco, Imamu alikua anamtukuza sana bibi huyo, Imamu Muhammad Jawaad (a.s) amekulia katika nyumba ya utume na uimamu, nyumba ambayo Mwenyezi Mungu ameitukuza, alilelewa na baba yake Imamu Ridha (a.s), ambaye alisimamia yeye mwenyewe malezi ya mtoto wake, alikua pamoja naye nyumani na safarini hadi akawa mkubwa, alipata elimu kubwa sana kutoka kwa baba yake, hadi akafikia kiwango cha kuwafundisha wanachuoni na wanafunzi njia za kusoma sheria za kiislamu, akawahimiza waandike na watunze anayo wafundisha, ambayo yeye alijifundisha kutoka kwa baba zake watakatifu.

Miongoni mwa majina yake ya sifa (laqabu) anaitwa: (Jawaad, Taqiyyu, Zakiyyu, Qaanii, Murtadhwa, Muntakhabu) na lililo mashuhuri zaidi ni (Jawaad) kutokana na wingi wa kutoa kwake na ukarimu wake, pia aliitwa mlango kusudiwa (babu muraad) baada ya kufa kwake kutokana na wingi wa kukidhiwa shida za watu wanapo kwenda kuomba kwenye kaburi lake tukufu, aliishi miaka (25) na muda wa uimamu wake ulikua ni miaka (17).

Kuhusu kisa cha kuzaliwa kwake na karama zilizo tokea, anasimulia bibi Hakimah mtoto wa Abu Hassan Mussa bun Jarafi (a.s) kua: Alipo karibia kujifungua Ummu Abu Jafari (a.s) Imamu Ridha aliniita na akaniambia: Ewe Hakimah nenda kaone anavyo jifungua, akaniingiza ndani (a.s) na akatuwashia taa, na akatufungia mlango, alipo anza kujifungua taa likazimika, na palikua na chombo, mimi nikashikwa na butwaa kwa kuzimika taa, kisha nikamuona Abu Jafari akiwa na chombo huku ana kitu laini kama ngua kinatoa mwanga mkali hadi nyumba nzima ikawa na mwanga.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: