Shehena ya vitabu tofauti vya kielimu na kitamaduni: Atabatu Abbasiyya tukufu yashiriki katika maonyesho ya vitabu ya kimataifa Bagdad…

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu imeshiriki katika maonyesho ya vitabu ya kimataifa yanayo fanyika Bagdad kupitia kitengo cha habari na utamaduni na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu, ambayo yameanza asubuhi ya Alkhamisi (11 Rajabu 1439h) sawa na (29 Machi 2018m) chini ya kauli mbiu isemayo (Tunasoma ili tuendelee) ambayo yana taasisi za usambazaji zinazo shiriki zaidi ya (600) za kitaifa na kimataifa.

Ushiriki huu sawa na ushiriki uliopita, Atabatu Abbasiyya tukufu imekuja na vitabu tofauti vinavyo husu watu wa tabaka zote, hivyo maonyesho haya ni sehemu ya mwendelezo wa mafanikio yaliyo patikana katika maonyesho yaliyo tangulia, ambayo huchukuliwa kua sehemu muhimu ya kukutana na ulimwengu wa nje, vitabu vinavyo onyeshwa vinaonyesha kiwango cha harakati za kitamaduni na kielimu kilichopo katika Atabatu Abbasiyya tukufu, jambo linalo onyesha upekee na ubunifu wa Ataba tukufu katika sekta ya utamaduni elimu na turathi vitu ambavyo vimeelezewa kisasa zaidi, nazo ni kazi halisi za Ataba tukufu kuanzia utunzi hadi uchapishaji, na hiyo ndiyo sifa ya pekee iliyopo katika Ataba ambayo matawi mengine hawana.

Kitengo cha habari na utamaduni, kinashiriki kikiwa na shehena ya vitabu mbalimbali vya dini, akhlaq, malezi, pamoja na vitabu vya kisekula, wakiwa pia na vitabu walivyo vifanyia uhakiki na kivichapisha katika muonekano mpya, vitabu walivyo navyo vinalenga watu wa tabaka zote na kila umri.

Huku kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu, nacho kimeonyesha machapisho yake na kazi zinazo fanywa na vituo vilivyo chini yake, kama vile (kituo cha turathi za Karbala, Hilla na Basra), machapisho yake ikiwa ni pamoja na Qur’an iliyo chapishwa na Maahadi ya Qur’an tukufu, pamona na misahafu ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Msimamizi mkuu wa maonyesho haya, Muhandisi Hashim Muhammad ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Hakika maonyesho haya ya vitabu yanafanyika baada ya jeshi letu na vyombo vya ulinzi na usalama kupata ushindi na kukomboa ardhi ya Iraq kutoka katika udhibiti wa magaidi wa Daesh, ushindi huo umethibikishia dunia kua raia wa Iraq wako imara katika vita na katika uandishi, kwa kutumia elimu tunaendelea na tunajenga kizazi chenye kujitambua, hakika maonyesho haya ni fursa nzuri kwa taasisi za usambazaji za Iraq kwani yanahusisha na kuthamini aina zote za vitabu vya fani zote zinazo endana na maendeleo ya dunia, hali kadhalika ni ujumbe wa amani na mapenzi kwa nchi zote duniani, hii inaonyesha kua Iraq inarudi katika nafasi yake kutokana na kufungua milango ya ushirikiano wa kielimu na kitamaduni na mataifa mengine kisha kutumia ushirikiano huo katika kujenga taifa.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imesha shiriki mara nyingi maonyesho ya kimataifa ya Bagdad na huyachukulia kua maonyesho muhimu kwake, pamoja na kushiriki katika maonyesho na makongamano mbalimbali yanayo fanyika ndani na nje ya Iraq, yanayo endana na sera yake ya kueneza fikra na mafundisho ya Ahlulbait (a.s), matawi yake hupata mwitikio mkubwa katika kila maonyesho.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: