Atabatu Abbasiyya inaishi katika mazingira ya furaha kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Ali (a.s)…

Maoni katika picha
Kama kawaida yake kila mwaka na katika siku tukufu kama hizi, Atabatu Abbasiyya tukufu na maeneo yanayo izunguka inaishi katika mazingira ya furaha, kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa (Yaasubu Dini) na kiongozi wa wacha Mungu na Wasii wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) Imamu Ali bun Abu Twalib (a.s) ambaye tarehe ya kuzaliwa kwake itasadifu siku ya Juma Mosi (13 Rajabu 1439h) sawa na (31 Machi 2018m).

Furaha hiyo inaonekana katika njia tofauti, Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba maalum inayo jumuisha vitu mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuupamba ukumbi wa haram tukufu kwa maua na mabango yenye ujumbe wa kuzaliwa kwake, hali kadhalika zimefungwa taa za rangi katika ukumbi wa haram tukufu, na sehemu zote za milangoni zimewekwa maua yenye muonekano mzuri, kuta za haram tukufu kwa nje zimepambwa kwa mataa za rangi zenye muonekano mzuri unao endana na tukio hili, pamoja na mabango yenye ujumbe murua, hali kama hiyo hiyo pia inaonekana katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu na katika mitaa inayo elekea katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kumbuka kua katika sherehe hizi kuna vitu vingine pia vitakavyo fanyika, miongoni mwa vitu hivyo ni: Ufunguzi wa mradi wa kituo cha kibiashara cha Afaaf, ufunguzi wa maonyesho ya bidhaa zinazo tengenezwa na Atabatu Abbasiyya tukufu yatakayo simamiwa na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu, pamoja na hafla zingine zitakazo fanywa na kitengo cha malezi na elimu ya juu pia kutakua na vitu vingine vingi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: