Mwaka wa tano mfululizo wa kufanyika kwa kongamano la wanachuoni wa kiislamu katika mji mkuu wa Pakistani Islamabad chini ya ushiriki wa Atabatu Husseiniyya na Abbasiyya tukufu.

Maoni katika picha
Kwa ushiriki wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya na uhudhuriji mkubwa wa wanachuoni wa madhehebu za kiislamu katika mji wa Islamabad leo Alkhamisi (29 Machi 2018m) sawa na (11 Rajabu 1439h), chuo kikuu cha Alkauthara kimefanya kongamano la tano la wanachuoni wa kiislamu chini ya ushiriki mkubwa wa vyombo vya habari, kongamano hili linafanyika kwa ajili ya kuondoa tofauti kati ya waislamu na kuweka ukaribu baina yao, katika kipindi hiki ambacho tunashuhudia mizozo, fitna na kufarakana kwa waislamu.

Kongamano lilifunguliwa kwa Qur’an tukufu iliyo somwa na msomaji na muadhini wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya Bwana Aadil Karbalai, kisha yakafuata mawaidha kutoka kwa mashekhe tofauti wa kiislamu, wote walisisitiza kujiepusha na mambo yanayo sababisha mfarakano katika jamii na ubaguzi baina ya waislamu, na wamehimiza kupambana na maadui wanao ingiza mbegu ya ubaguzi katika uislamu, na wanataka kuudhofisha umoja wa waislamu kwa ajili ya kufikia malengo yao ya kishetani, wazungumzaji wote wamesema kua; wanachuoni wa kishia wana nafasi kubwa sana katika kulinda dini ya kiislamu, kutokana na msimamo wa Marjaiyya kwa miaka mingi, hakika fatwa yake ilibadilisha mtazamo wa jamii nzima ya kiislamu na wasio kua waislamu duniani kote, namna alivyo onyesha kuzijali familia za ndugu zetu waumini wa madhehebu ya sunni wanao ishi katika miji iliyo kua na vita, kaskazini na magaribi ya Iraq sambamba na kuzilinda na kuzihami familia zisizo kua za kiislamu katika maeneo hayo na kote nchini Iraq, pia wazungumzaji walisisitiza kua miongoni mwa wajibu wa wasomi wa dini ni kupambana na uvumi unao lenga kuchafua dini ya kiislamu, kuna mambo yanayo ingizwa katika uislamu kwa lengo la kuharibu haiba na muonekano wa uislamu katika jamii na kwa vizazi vijavyo, tena mambo hayo yanafanywa kwa mtazamo wa mbali.

Kuhusu ujumbe ulio wasilishwa na Sayyid Muhammad Ali Halo kutoka katika hauza ya Najafu Ashrafu, ambaye aliongea kwa niaba ya ugeni wa Ataba mbili tukufu alisema kua:

Yatupasa kuashiria baadhi ya mambo muhimu katika kongamano hili tukufu, tukiwa katika chuo kikuu cha Alkauthar jambo hili linaonyesha umuhimu wa kongamano hili, mambo muhimu ninayo penda kuyataja kwenu, miongoni mwake ni yale yanayo shambulia jamii ya kiislamu ya leo, mashambulizi ya kigaidi yanayo lenga kututenganisha, kuna ulazima wa kusimama pamoja kama waislamu na kupambana na kundi hili, aidha tunatakiwa kuendeleza vikao vya aina hii vinavyo jenga fikra za kupambana na ubaguzi pamoja na ugaidi.

Akabainisha kua: Leo hii sekta ya habari imekua nyenzo kubwa ya kujenga mitazamo ya watu, yatupasa kupambana na vyombo vya habari vinavyo potosha dini ya kiislamu na kuifanya ionekane kua ni dini ya chuki na ugaidi, sambamba na kupambana na wale wanaojifanya wanatangaza dini wakati wanavunja misingi ya dini ya kiislamu ili jamii isiingie katika maovu.

Akamaliza kwa kusema kua: Tunawashukuru kwa mkusanyiko huu mtukufu, na tunakufikishieni maelekezo ya Marjaa dini mkuu Mheshimiwa Ayatullah Sayyid Ali Husseini Sistani, ambaye amehimiza umuhimu wa kushikamana na kujiepusha na mifarakano, nimesha toa maelezo ya wazi kuhusu hilo, maelezo yote niliyo toa yanatokana na fatwa tukufu iliyo mwagiliwa kwa damu za raia wa mikoa ya kusini walipo miminika kwenda kuwaokoa ndugu zao waishio katika miji ya magharibi.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu aineemeshe miji ya waislamu, kwa kuwapa heri nyingi na afya na awaepushe na kila linalo haribu umoja wa waislamu hakika yeye ni msikivu na mjibuji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: