Kutokana na kufikisha umri wa kuwajibikiwa na sheria: Atabatu Abbasiyya tukufu yafanya hafla ya kuwapongeza wanafunzi wa shule za Ameed…

Maoni katika picha
Chini ya kauli mbiu isemayo: (Utukufu wangu ni kumtii Mola wangu) na kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s), Atabatu Abbasiyya tukufu chini ya usimamizi wa kitengo cha malezi na elimu ya juu imewafanyia hafla wanafunzi (360) wa shule za Ameed, katika ukumbi wa jengo la Kuleini asubuhi ya leo Ijumaa (12 Rajabu 1439h) sawa na (30 Machi 2018m) iliyo kua na mahudhurio makubwa ya viongozi, akiwemo mkuu wa idara ya malezi ya Mkoa, na jopo la wajumbe wa kamati kuu ya uongozi wa Ataba tukufu pamoja na wasimamizi wa wanafunzi.

Baada ya Qur’an ya ufunguzi na wimbo wa taifa pamoja na wimbo wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ulifuata ujumbe wa rais wa kitengo cha malezi na elimu ya juu Dokta Abbasi Didah, miongoni mwa aliyo sema ni: “Falsafa ya malezi inayo fatwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, inatoa picha ya ujumbe mtukufu wa mbinguni (Mwenyezi Mungu) unao fafanuliwa na vitabu pamoja na Mitume, ujumbe ambao humfikisha mwanadamu katika kilele cha amani na uongofu, sambamba na kubeba majukumu ya kufanya vitendo vizuri na kua na maadili mema”.

Akaongeza kusema kua: “Mahafali hii ni ya kihistoria, ni mahafali ya kuingia katika umri wa balekhe, umri ambao mwanadamu huanza kuwajibikiwa na sheria, na hapo hutakiwa ashikamane na utekelezaji wa hukumu za dini, kama vile swala, ambayo ni ibada inayo mlinda na mambo machafu na maovu, ashikamane na hijabu, huo ni wakati wa kushikamana na amri zote za Mwenyezi Mungu mtukufu na kufanyia kazi kauli yake isemayo (Na wala sikuwaumba majini na binadamu ispokua waniabudu) mwanamke anapo jistiri hua ni ngao imara ya kulinda jamii, ukizingatia kua mwanamke ndiye msingi wa familia njema iliyo shikamana na mafundisho ya dini tukufu, pia husaidia kuzuia fikra potofu zinazo lenga kuvunja uaminifu wake na kumuweka mbali na Mwenyezi Mungu mtukufu na kisha kuipotosha jamii kwa ujumla”.

Akamaliza kwa kusema: “Yatupasa tuwapongeze wanao tushika mikono na kutupeleka katika utumishi mtukufu wa Abulfadhil Abbasi (a.s), na inatulazimu kuonyesha shukrani zetu kwa kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa kutambua mtazamo wa Ataba na viongozi wake pamoja na malengo yao na kuyafanyia kazi kwa vitendo, yatupasa tuushukuru uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya kwa maelekezo yao, na tushukuru fikra hii tukufu inayo tekelezwa na viongozi wa shule za wasichana kwa juhudi za walimu na viongozi wa idara ya malezi, pia shukrani za pekee ziwaendee Hashdi Sha’abi na fatwa tukufu ya kujilinda, kama sio wao tusinge weza kulinda heshima ya mwanamke wala kutoa malezi mema au kufundisha, na shukrani zote zimuendee Mwenyezi Mungu mtukufu”.

Hafla ya leo imeshuhudia kupewa zawadi kwa kundi la wanafunzi, pia kulikua na ratiba mbalimbali, ikiwa ni pamoja na uimbaji wa kaswida za kimashairi na maigizo na mwisho kabisa wanafunzi wakapewa zawadi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: