Kamati inayo simamia shughuli ya ufunguzi wa kituo cha kibiashara cha Afaaf, na maonyesho ya shughuli zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza kukamilika kwa maandalizi ya maonyesho hayo yatakayo anza asubuhi ya kesho Juma Mosi (13 Rajabu 1439h) sawa na (31 Machi 2018m).
Kwa mujibu wa taarifa ya kamati, shughuli hii inafanywa sambamba na kumbukumbu ya kuzaliwa kwa kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s), na itakua na sehemu mbili, sehemu ya kwanza: Ufunguzi wa kituo cha kibiashara cha Afaaf, ambacho ni miongoni mwa miradi ya kiuchumi ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika mkoa wa Karbala. Mradi huu umejengwa katika kitongoji cha Hussein (a.s), kwenye eneo lenye ukubwa wa (2m2600) na jengo lake lina ghorofa tatu, na lina sehemu mbili, sehemu ya maduka, na sehemu nyingine ni maofisi na magodauni, kinachukuliwa kua kituo bora katika mkoa wa Karbala, kwani kimejengwa kisasa zaidi, na kinaendana na maendeleo ya soko la sasa, kitahudumia wakazi wa Krabala na mazuwaru watukufu, kitakua na nafasi kubwa ya kibiashara na kitafungua milango yake kwa mara ya kwanza kikiwa na bidhaa halisi na sio feki, jambo hili limetiliwa umuhimu kuanzia katika usanifu wa jengo.
Shughuli ya pili itakayo fanyika, ni maonyesho ya shughuli zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, kupitia miradi yake ya kiutamaduni, kiuchumi na kiutumishi, maonyesho hayo yatafanyika chini ya kauli mbiu isemayo: (Miradi yetu inashajihisha uwezo wa taifa) asilimia kubwa ya vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu vitashiriki, vitakua zaidi ya vitengo 25, kwa ajili ya kuwaonyesha wananchi na mazuwaru watukufu pamoja na taasisi za serikali na zile za binasfi huduma zinazo tolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu, na kwa upande mwingine kuonyesha maendelea na mafanikio yaliyo fikiwa na Ataba tukufu yanayo chuana na makampuni makubwa ya kimataifa.