Sayyid Ahmadi Swafi: Turathi ni utambulisho wa kujivunia, umma bila turathi ni sawa na umma ulio katikiwa nasabu…

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi amesisitiza kua, turathi ni utambulisho wa kujivunia, na umma usiokuia na turathi ni umma ulio katikiwa nasabu, turathi hizi za wino wa wanachuoni sio kwamba tunajivunia tu lakini tunatukuzwa kwa sababu yao, kama si wao tusingekua katika hali hii.

Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya turathi ya mwaka wa kwanza, yenye kauli mbiu isemayo (Turathi zetu ni utambulisho wetu) yanayo simamiwa na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu.

Miongoni mwa aliyo sema ni: “Ni mengi kiasi gani yaliyo andikwa na watu wa mwanzo, na yana uzuri ulioje na utukufu kiasi gani mambo waliyo fanya katika mazingira magumu, walikua wanathamini wanacho andika kushinda wanacho kula, historia imejaa turathi zetu tunazo jivunia, mwanafunzu atakapo jivunia masomo ya dini anaweza kupata nasaha kutoka kwa walimu walio mtangulia, wanaweza kumuambia! Soma historia ya wanachuoni walio kuwepo kabla yako, hakika kusoma huko kunaweza kukufanya ushikamane na ulicho nacho, na utaona namna walivyo jitolea walio kua kabla yako ili sisi tuweze kusoma kwa urahisi hivi sasa, baadhi ya tunayo yasoma kuhusu watu wa mwanzo inakua vigumu kuyaamini japo ni mambo yaliyo tokea, sio kosa lao ni kosa letu tutakapo shindwa kuelewa mazingira magumu waliyo pitia wanachuoni watukufu”.

Akaongeza kusema kua: “Tunapo angalia baadhi yao walikua hawamiliki hata pesa ya kununua mafuta ya taa lake, walikua wanaenda katika maeneo ya umma na kujisomea huko, na wengine walikua wanakesha kwa kusoma kwenye mwanga wa mwezi, ukweli ni kwamba unaweza kusoma kwa shida kubwa katika mwanga wa mwezi kiasi kwamba macho yatapata taabu sana, lakini walikua wanasoma hivyo hivyo”.

Akasisitiza kua: “Turathi hizi za wino wa wanachuoni sio kwamba tunajivunia tu, bali tunatukuzwa kwa sababu yao, kama si wao tusingekua katika hali hii, pamoja na wino hizo pia wanachuoni hao walimwaga damu zao kwa ajili ya kutetea haki na uandishi wao, tukitaka kutaja wanachuoni walio uawa orodha itakua ndefu sana, wengi wao walipo andika waliuawa lakini wakawa wametuachia matunda makubwa ya kielimu, hadi leo hauza zinashuhudia walicho kiandika, haya tunayo yaona yamefanywa na watu wa mwanzo na yaliyo potea ni mengi zaidi, tunatakiwa kukamilisha kazi zilizo fanywa na watu wa mwanzo kwa kufanya utafiti katika historia na kuihifadhi inaweza kua ni miongoni mwa majukumu yetu”.

Akafafanua kua: “Imamu Swadiq (a.s) alikua anapo pita kwa baadhi ya maswahaba wa Imamu Baaqir (a.s) alikua anasema: Kama sio hawa athari za baba yangu zingepotea.. ukweli ni kwamba kama sio wanachuoni athari zetu zingepotea, na kama sio wanachuoni wa sasa ambao kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mtukufu bado wanaendelea kutufundisha historia hiyo na kutuonyesha utukufu wa watu wa mwanzo, kupitia kusoma walicho kiandika, kwa hakika turathi ni utambulisho wa kujivunia, umma usio kua na turathi ni sawa na umma uliokatikiwa nasabu hapa duniani, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mtukufu tangu kabla ya miaka mia moja, zimeandikwa historia tunazo jivunia leo hii, tandu ilipo kua Bagdad ndio kitovu cha elimu wakati wa Shekh Kuleini na Shekh Mufidi na Shekh Tusi, au wakati ilipo kua Najafu na bado inaendelea kua kitovu cha elimu kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mtukufu, huenda baada ya chini ya miaka kumi historia ya Najafu itafikisha miaka elfu moja kuanzia alipo hamia Shekh Tusi katika mji huo, miaka hiyo elfu moja itazungumzia mazingira ya kielimu kwa kulinganisha na mji wa Hilla, Karbala, na Qum pamoja na miji mingine ya kielimu kote duniani, tunashukuru kwa yote yaliyo andikwa katika vitabu, lakini inawezekana mambo ambayo bado hayaja andikwa ni mengi kushinda yaliyo andikwa”.

Akaendelea kusema: “Natoa wito kwa ndugu wote watukufu.. mwanadamu anaye shughulika na historia (nakusudia turathi) kwa hakika anashughulika na watu walio mwamini Mwenyezi Mungu, baadhi ya vijana wa leo wanaweza wasifahamu umuhimu wa yaliyo andikwa na watu wa zamani na juhudi kubwa walizo tumia, tunapo soma maisha ya baadhi yao, kwa uhakika tunakosa maneno yanayo lingana na heshima kubwa waliyo kua nayo kwa kufanya kazi tukufu katika maisha magumu yasiyo kua na utulivu, wakiwa na maradhi, ufakiri pamoja na mitihani mingine mingi, walikua hawakati tamaa, walikua na msimamo mkubwa katika kusimamia malengo yao”.

Akabainisha kua: “Leo tunashuhudia watu wengi wanajishughulisha na turathi, yawezekana miongoni mwetu wapo walio tumia miaka mingi katika umri wao na wamezizawadia maktaba za kiislamu athari nzuri, sitakoseo nikisema kua Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Ashkuri (M/M ampe umri mrefu) ana mchango mkubwa katika swala hili, ni mwalimu wa fani hii, nimemtaja mbele yake, namshukuru Mwenyezi Mungu, kuna wanachuoni wengi wamenufaika naye na wamesambaa ehemu mbalimbali”.

Akasema kua: “Atabatu Abbasiyya tukufu imechukua jukumu la kufanya utafiti wa turathi katika mikoa mitatu, lakini hatutaishia hapo, huu ni mwanzo wa kuendelea na utafiti sehemu zingine pia, kwa kweli tunapokea maombi mengi ya watu wanaotaka tuiingize mikoa yao katika ratiba hiyo, sawa iwe katika historia ya turathi za Karbala au Hilla au Basra, vituo vivyo vitatu vipo tayali na Mwenyezi Mungu awalipe heri ndugu wanao fanya kazi katika vituo hivyo kwa juhudi kubwa wanayo fanya ya kuibua turathi zilizopo na kuzitanbulisha kwa ajili ya kunufaika nazo”.

Akaongeza kusema kua: “Tunafurahi sana kwa kuhudhuria kwenu katika maonyesho haya kwa ajili ya kuangalia baadhi ya kazi zilizo fanywa na dhugu zetu, jambo muhimu ni kwamba tunahitaji sana tuzijali turathi kwa kiwango cha juu, nazungumzia turathi za kielimu, na sisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu tupo tayali kupokea ushauri wowote au kushirikiana na juhudi yeyote, tupo tayali kuwahudumia, tunahisi jukumu hili ni lazima tulitekeleze kwa kiasi tutakacho weza, mji wa Najafu Ashrafu, Karbala na Hillah ii ni miji muhimu, ninaamini kua hizi turathi tulizo nazo zinahitaji watu wa kuzitambulisha, kuna taasisi za watu binafsi zimeanza kuonyesha kujali swala la turathi na wanaendelea vizuri.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: