Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu chazindua maonyesho ya mwaka wa kwanza chini ya kauli mbiu isemayo (Turathi zetu ni utambulisho wetu)…

Maoni katika picha
Kitenge cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu alasiri ya Ijumaa (12 Rajabu 1439h) sawa na (30 Machi 2018m) kimezindua maonyesho ya mwaka wa kwanza chini ya kauli mbiu isemayo (Turathi zetu ni utambulisho wetu), katika ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) ndani ya Ataba tukufu, na kuhudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi pamoja na katibu mkuu Muhandisi Muhammad Ashiqar, na jopo kubwa la wasomi wa hauza na sekula, ikiwa ni pamoja na kundi kubwa la wadau wa sekta ya turathi.

Hafla ya ufunguzi ilianza kwa Qur’an tukufu kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ukaimwa wimbo wa taifa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya, halafu ukafuata ujumbe wa kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, miongoni mwa aliyo sema ni: “Hakika turathi ni utambulisho tunao juvunia, umma bila turathi ni sawa na umma uliokatika nasabu, turathi za wino wa wanachuoni sio kwamba tunajivunia tu bali tunatukuzwa kwa sababu yao, kama si wao tusinge kua katika hali hii..).

Baada yake ukafuata ujumbe wa mhakiki mkubwa Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Hussein Ashkuri, ambaye alisema kua: “Tunamiliki hazina kubwa ya turathi na kuna juhudi kubwa ya kuitoa na kuidhihirisha, jambo hili lilikua linaendelea vizuri, lakini mabadiliko ya hali ya siasa yameathiri jambo hili, kwa mfano maafa yanayo tokea yanasababisha kuharibika kwa turathi nyingi zilizopo katika maktaba za serikali na binafsi, nimeona nakala kale nyingi katika utafiti wangu ambazo hazija fikiwa na mtu yeyote, nimeandika orodha kubwa na nilianza kukusanya kwanza hazina za kiislamu kisha nikafungua kituo cha kuhuisha turathi za kiislamu, na nikaanza kupiga picha nakala kale zilizopo katika maktaba za serikali na binafsi, hadi sasa tumesha kusanya picha za nakala kale zaidi ya laki mbili”.

Akaongeza kusema kua: “Jambo linalo sikitisha ni kwamba watu wengi wanafikiria kua Shia hatuna turathi nyingi, ni mafakiri wa elimu, wakati ukifanya utafiti wa nakala kale zinathibitisha kua sisi ni matajiri wa turathi, nazipongeza sana harakati zilizo anza miaka kumi ya mwisho hapa Iraq, pia nazipongeza Ataba tukufu kwa kuhuisha turathi nyingi muhimu, kila siku naona kitabu kipya na kinachapiswa kwa umakini mkubwa hii ni ishara njema, mimi napongeza sana juhudi anazo fanya ndugu yetu mtukufu Sayyid Ahmadi Swafi katika sekta hii, tunamuombea mafanikio mema yeye na kila anaye fanya kazi katika sekta hii”.

Baada yake ukafuata ujumbe wa mkuu wa maktaba ya Maimamu wawili (Jawadaini) Sayyid Ayadi Shaharistani, miongoni mwa aliyo sema ni: “Hakika turathi tulizo achiwa na wanachuoni ni hazina ya kujivunia na ngazi inayo tufikisha katika kilele cha utukufu, tutapongezwa na umma zingine na kuziangazia ziweze kujua walio pita kupitia historia za wanachuoni watukufu, jambo la kufurahisha zaidi ni pale tunapo ona Atabatu tukufu miongoni mwa huduma zake mbalimbali kwa jamii, inalipa umuhimu mkubwa jambo la elimu na turathi, vikao hivi na nadwa mbalimbali ni ushahidi wa wazi wa namna Atabatu Abbasiyya tukufu inavyo jali jambo hili, wametenga siku maalumu katika ratiba yao ya kumzungumzia mmoja wa vinara wa umma huu ambaye ni Sayyid Hibatu-Dini Alhusseini ajulikanaye kama Shaharistani, ambaye tutamkumbuka kwa mara ya hamsini, hakika vikao hivi vya kielimu vina athari kubwa sana katika kushea maarifa na kuhuisha turathi za umma wetu, jambo hili tunaliona kwa ujumla katika Atabatu Abbasiyya tukufu na kwa namna ya pekee katika kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu, kupitia ushirikiano endelevu na kubadilihana mawazo na mitazamo kwa kufuata mwenendo sahihi wa kielimu”.

Kisha ukafuata ujumbe wa maktaba ya Baitul-Hikma, ulio wasilishwa na Dokta Ismaiil Jaabir ambaye alisema kua: “Hakika jambo hili linalo fanywa na kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu ni jambomuhimu sana, linatilia umuhimu mambo yaliyo pita na kuhifadhi turathi za kiarabu na kiislamu, kinacho fanywa na Atabatu Abbasiyya ni muhimu sana, kulinda turathi zisiharibiwe na kupotea”.

Masikio ya wahudhuriaji yakaburudishwa kwa kusikiliza shairi lililo somwa na Dokta Aadil Baswiswi, na kufuatiwa na kugawa zawadi kwa wasomi wanaojishughulisha na turathi, kisha watu wote wakiongozwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu wakaelekea katika ufunguzi wa maonyesho yanayo fanyika katika eneo lililo ezekwa katikati ya harama mbili tukufu, katika maonyesho hayo kimeshiriki kituo cha turathi cha (Barsa, Hilla na Karbala) pamoja na Maahadi ya Qur’an tukufu iliyo chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: