Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Muhammad Ashiqar amehudhuria katika hafla ya uzindizi pamoja na idadi kubwa ya wajumbe wa kamati ya uongozi na marais wa vitengo, palikua pia ugeni rasmi ulio wakilisha Atabatu Husseiniyya tukufu, bila kusahau wawakilishi wa serikali ya mkoa mtukufu wa Karbala wakiongozwa na Muhandisi Jaasim Khatwabi rais wa baraza la mkoa na idadi kubwa ya wageni waalikwa kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala.
Hii ni mara ya kwanza kufanyika maonyesho kama haya na Atabatu Abbasiyya tukufu, yanayo lenga kuwaonyesha wananchi na mazuwaru watukufu pamoja na taasisi binasfi za serikali, shughuli zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika sekta mbalimbali, pamoja na huduma wanazo toa kwa mazuwaru watukufu, na kwa upande mwingine maonyesho haya yanalenga kuonyesha maendeleo yaliyo fikiwa na Atabatu Abbasiyya, ambapo bidhaa zake zinachuana na bidhaa zinazo zalishwa na makampuni makubwa ya kimataifa na zinachangia uchumi wa taifa na ukuaji wa viwanda vya ndani.
Katika maonyesho haya ambayo ushiriki wake umepangwa kulingana na shughuli za kila tawi (kitengo), matawi au vitengo vinavyo shiriki ni:
- - Hospitali ya rufaa Alkafeel.
- - Shirika la teknolojia ya kilimo cha kisasa Aljuud.
- - Kiwanda cha Atabatu Abbasiyya tukufu cha kutengeneza milango na madirisha ya makaburi na mazaru (sehemu za kuhistoria).
- - Shiruka la uchumi Alkafeel.
- - Kiwanda cha Waahah cha kutengeneza chakula cha kuku.
- - Kitengo cha zawadi na nadhiri.
- - Darul-Kafeel inayo husika na uchapishaji na usambazaji.
- - Kitengo cha uangalizi wa kihandisi.
- - Kitengo cha miradi ya kihandisi.
- - Idara ya mawasiliano ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
- - Kitengo cha habari na utamaduni.
- - Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu.
- - Maahadi ya Alkafeel ya kukuza elimu na kuendeleza vipaji.
- - Kituo na studio cha Aljuud inayo husika na picha zinazo cheza.
- - Kituo cha Alkafeel cha uchapishaji wa namba na matangazo.
- - Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji.
- - Idara ya fikra na ubunifu.
- - Kituo cha kimataifa cha utafiti na masomo Al-Ameed.
- - Mtandao wa kimataifa Alkafeel.
- - Shirika la ujenzi Liwaau lililo chini ya kitengo cha miradi ya kihandisi.
- - Kitengo cha utumishi, kimewakilishwa na kamati ya vitalu vya Alkafeel pamoja na mradi wa nyuki wa Alkafeel.
- - Shirika la Nurul-Kafeel linalo tengeneza bidhaa za wanyama na vyakula.
- - Kitengo cha malezi na elimu ya juu, kimewakilishwa na shule za Ameed pamoja na chuo kikuu cha Al-Ameed.
- - Kituo cha Alkafeel cha utengenezaji wa kazi za kitalamu.
- - Mradi wa Alkafeel wa kuku na uanguaji wa mayai.
- - Idara ya Alkafeel ya kunufaika na mitambo (magari) na utalii wa kidini.
- - Maahadi ya turathi za mitume ya masomo ya hauza ya kielektronic.
- - Shirika la Alkafeel la usalama na mawasiliano.
- - Watamu wa Alkafeel wa mafunzo ya huduma za uokoaji katika vita.
Hali kadhalika kuna ushiriki wa baadhi ya mashirika ya kitaifa yanayo changia ujenzi wa taifa, kama vile shirika la Itihaad na Al-Qaalib.
Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kufuatia kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Ali (a.s), leo tumezindua mradi muhimu sana, nao ni kituo cha kibiashara cha Afaaf, ambacho kimetupa fursa ya kufanya maonyesho ya shughuli zinazo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu, pamoja na bidhaa zinazo tengenezwa na vitengo vyake ambazo ni matunda halisi ya kazi za wairaq, zinazo thibitisha uwezo wa raia wa Iraq wa kupambana na matatizo iwapo wakiwezeshwa, kupitia mkusanyiko huu nawaambia wananchi wa Iraq kua; Iraq ni taifa hai lenye uwezo wa kuzalisha pamoja na matatizo yote iliyo pitia, na linaweza kushinda vikwazo vyote”.