Kwa mnasaba wa kumbukumbu ya kuzaliwa baba yao: Bendera mbili ya Imamu Hussein na Abulfadhil Abbasi zainawirisha mbingu ya Rawalbandi Pakistani.

Maoni katika picha
Mashairi na maneno mazuri yameongelewa katika taasisi ya (Haamilu Raayah) katika moja ya miji kongwe ya Pakistani.. Rawalbandi, katika kusherehekea mazazi wa bwana wa mawasii kiongozi wa waumini (a.s).

Hafla ya mwaka huu (1439h) imefanywa mbele ya wageni kutoka katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya ambao walialikwa kwa ajili hiyo.

Hafla ilianza baada ya swala ya Dhuhurain katika msikiti wa taasisi, na adhana ilisomwa na muadhini wa Ataba mbili tukufu bwana Aadil Karbalai.

Baada ya kumaliza hafla, wageni waligawa zawadi za tabaruku kwa wahudhuriaji, kisha wote wakaelekea katika kupandisha bendera ya Imamu Hussein (a.s) baada ya kuimba wimbo wa Atabatu Husseiniyya tukufu na kusoma dua, chini ya furaha kubwa za wahudhuriaji na machozi ya unyenyekevu.

Kisha katibu mkuu wa taasisi hiyo akakabidhiwa bendera ya Abulfadhil Abbasi (a.s), itakayo pandishwa baada ya kukamilika ujenzi wa mnara wake unao jengwa katika uwanja wa msikiti.

Kumbuka kua shughuli hizi zinafanyika baada ya kumalizika kongamano la msimu wa Karbala (Nasimu Karbala) ambalo husimamiwa na Atabatu Husseiniyya tukufu na ushiriki wa Atabatu Abbasiyya tukufu Pakistani kwa mwaka wa tano mfululizo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: