Tarehe kumi na tano Rajabu, ni siku ya huzuni kwa kufariki ulimi wa mwana harakati za Husseiniyya bibi Zainabu (a.s)…

Maoni katika picha
Tarehe kumi na tano Rajabu umma wa kiislamu huingia katika huzuni ya kukumbuka kifo cha Kaaba ya huzuni na mama wa misiba, jabali la subira Aqilah bani Hashim na ulimi wa mwana harakati bibi Zainabu Kubra (a.s).

Bibi Zainabu (a.s) alikua na elimu bila kufundishwa, alikua anafahamu bila kufahamishwa, alkua na akili ya hali ya juu, alikua mfasaha, mwenye kuipa nyongo dunia, mwenye kufanya ibada kwa wingi kama baba yake kiongozi wa waumini na mama yake Zaharaa (a.s), alisifika kwa mazuri mengi (a.s), alisoma kwa baba yake na kaka zake, na alikulia katika nyumba tukufu ya ma-alawi, alikua mwanamke mtukufu wa pili baada ya mama yake Zaharaa (a.s), uhai wake ulijaa utukufu na karama, aliishi katika utukufu ulio jaa heshima.

ZAINABU (A.S) NI ULIMI WA MAPINZUZI UZUNGUMZAO.

Imamu Hussein (a.s) alikua anajua njama za maadui zake za kudanganya watu na kuwapotosha, na baada ya kufahamu kua baada ya kuuawa kwake watapotosha ukweli wa harakati yake tukufu, ilikua ni muhimu aandae mtu atakaye pambana na upotoshaji wa utawala wa Umawiyya, hivyo (a.s) alikua anamuelezea dada yake malengo ya harakati yake na njama za watawala wa Umawiyya, pamoja na kumfafanulia jukumu lao kwa waislamu, tangu walipo ondoka katika mji wa Madina hadi walipo kutana na makundi ya mahujaji.

Kisha katika safari ya kwenda Iraqi hadi walipo fika Karbala, aliendelea kumuelezea dada yake kila kitu hadi alipo fikwa na umauti (a.s), hakughafirika hata wakati mmoja kumuelezea njama za utawala wa Umawiyya, na umuhimu wa kuendeleza malengo ya harakati yake tukufu, kwa sababu kuendelea kutangaza malengo ya harakati yake baada ya kifo chake ni muhimu sana sawa na mapambano yenyewe, na chaguo lake la mtu atakaye endeleza mapambano baada yake lilikua ni bibi Hauraa (a.s), kwa kua pamoja naye katika safari hii ya jihadi, yeye ni mbegu itokanayo na bwana wa ufasaha iliyo jaa hekima na ufasaha.

Zainabu alikua wa pekee kwa ulimi wa baba yake kiongozi wa waumini.

katika wakati mgumu na chini ya ulinzi wa madhalimu, alikua ni mtu wa kupigiwa mfano katika ushujaa na maneno yaliyo jaa hekima na ujasiri ya kuwa aibisha watawala, aliendesha safina ya harakati tukufu na kuzibakiza milele, miongoni mwa harakati zake (a.s) zinazo simuliwa katika historia ni khutuba aliyo toa katika majlis ya Yazidi.

Pale alipo sema: “Ewe Yadidi hivi ulidhani kututembeza kila kona ya ardhi, chini ya jua, tukawa tunapelekwa kama mateka, kua tumekua madhalili mbele ya Mwenyezi Mungu, na wewe umekua mtukufu, hiyo ndio ilikua dhana yako kubwa, umepata hasara, umeona furaha, dunia inavyo kuendea vizuri, na mambo yamenyooka, baada ya kupewa ufalme, subiri, umesahau kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo: “Wala wasidhani wale wanao kufuru kwamba huu muhula tunao wapa ni kheri kwao. Hakika tunawapa muhula wazidi madhambi. Na yao wao ni adhabu ya kuwadhalilisha”.

Fanya vitimbi vyako, fanya utakalo, tumia juhudi zako, Wallahi hautafuta utajo wetu, wala hauta uwa ujumbe wetu, wala hauta pata aibu zetu, Je! Umeona ispokua udhaifu (wako), na siku zako zinahesabika, na kundi lako litatawanyika, siku atakapo nadi mwenye kunadi, Laana ya Mwenyezi Mungu ipo juu ya madhalimu”.

Kifo chake

Wana historia wametofautiana kuhusu mwaka wa kifo chake (a.s), kauli yenye nguvu ni ile isemayo kua alikufa mwaka wa (62h), lakini wengine wanasema kua alikufa mwaka wa (65h).

Anaitwa mama wa misiba, ni haki aitwe hivyo, alishuhudia kifo cha babu yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), na msiba wa kifo cha mama yake Zahara (a.s) pamoja na mitihani aliyo pata, na msiba wa kifo cha baba yake kiongozi wa waumini (a.s) pamoja na mitihani aliyo pata, na msiba wa kifo cha kaka yake Hassan (a.s) kwa sumu, pamoja na msiba mkubwa wa kuuawa kwa kaka yake Hussein (a.s) kuanzia mwanzo hadi mwisho, na kuuawa kwa watoto wake Aun na Muhammad pamoja na mjomba wao mbele ya macho yake, na akachukuliwa mateka kutoka Karbala hadi Kufa, akaingizwa kwa maluuni ibun Ziyadi katika kikao cha wanaume, wakampokea kwa kejeli na dharau, kisha akatolewa Kufa na kupelekwa Sham akiwa na kichwa cha kaka yake pamoja na vichwa vya watoto wake na vichwa vya watu wa familia yake vikiwa vimetungikwa katika mikuki mirefu njia nzima, hadi walipo fika Damascus wakiwa katika hali hiyo, wakaingizwa kwa muovu Yazidi katika kikao cha wanaume.

Amani iwe juu yako ewe bibi yangu na kiongozi wangu ewe mama wa misiba Zainabu Kubra, siku uliyo zaliwa na siku uliyo kwenda kwa Mola wako ukiwa umeridhia na umeridhiwa na siku utakayo fufuliwa na kua hai.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: