Kwa nyoyo zilizojaa huzuni Maukibu ya pamoja ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya wanatoa taazia kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika kumbukumbu ya kifo cha bibi Zainabu (a.s)…

Maoni katika picha
Kwa nyoyo nyenyekevu zilizo jaa huzuni na maneno yanayo toka katika vinywa vya wapenzi wa Muhammad na watu wa nyumbani kwake watakatifu na ndani ya ukumbi wa haram ya mbeba bendera na mtumishi wa Hauraa Abulfadhil Abbasi (a.s), Maukibu ya watumishi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya inayo jumuisha viongozi na watumishi wa Ataba hizo tukufu siku ya leo (15 Rajabu 1439h) sawa na (02 Aprili 2018m) wamefanya matembezi ya kumuomboleza Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kutokana na tukio la kufariki kwa Aqilah bibi Zainabu (a.s).

Matembezi hayo yameanzia katika ukumbi wa haram ya Alkafeel Abulfadhil (a.s) na kupitia katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu, wakati wa matembezi hayo ziliimbwa kaswida za kuomboleza zilizo amsha huzuni kutokana na msiba huu mkubwa, na walipo fika katika malalo ya bwana wa vijana wa peponi Imamu Hussein (a.s), walipokelewa na ndugu zao watumishi wa Atabatu Husseiniyya tukufu, wakaimba na kufanya majlisi ya maombolezo iliyo elezea dhulma alizo fanyiwa bibi Hayraa Zainabu (a.s).

Maikibu zilianza kumiminika katika Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya tangu jana hadi leo zikija kutoa pole kwa Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kufuata utaratibu ulio wekwa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika kumbukumbu ya kifo cha bibi mtakatifu Hauraa Zainabu (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: