Atabatu Abbasiyya tukufu yafanya hafla ya kuwapongeza wanafunzi wateule wa Sekondari (1300) katika mkoa wa Muthanna na kuwashajihisha na kuipongeza sekta ya malezi na elimu ya Iraq…

Maoni katika picha
Chini ya usimamizi wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kituo cha Murtadha cha utamaduni na maelekezo kimefanya hafla ya mwisho wa mwaka kwa ajili ya kuwapongeza wanafunzi walio faulu kuendelea na elimu ya sekondari wa wilaya ya Ramitha na vitongoji vyake katika mkoa wa Muthanna, inatokana na Atabatu Abbasiyya kuamini umuhimu wa kusaidia sekta ya malezi ya Iraq, na kushajihisha wanafunzi walio faulu kuendelea na masomo ikiwa ni pamoja na kuwajengea kujiamini katika safari wao ya elimu.

Hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ukaibwa wimbo wa taifa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya tukufu, baada ya hapo ukafuata ujumbe wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu ulio wasilishwa na Shekh Muhammad Kuraitwi, miongoni mwa aliyo sema ni: “Hakika kuteuliwa ni jambo zuri na linapendeza kwa kila mtu, inapendeza zaidi itakapo kua kuteuliwa huko kunatokana na maendelea mazuri ya elimu, mwanafunzi aliye teuliwa hutegemewa na watu wote kwani ndiye anaye tengeneza mustaqbali, kusema kweli mchango wenu uko wazi katika kila kitu, nakusudia watoto wa mkoa huu, walionyesha msimamo wa pekee na mmekua fahari kubwa kwetu katika ujenzi wa taifa, nyie wanafunzi wa leo mnao mfano mzuri wa kuiga sio tu katika elimu bali hata katika jihadi, sisi tunakuungeni mkono na tunasimama pamoja na nyie, tunakusaidieni kwa hali na mali, na tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awajaalie kua viongezi wa baadae, mtakao peperusha bendera ya elimu, tabia njema na dini, hili litawezekana kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mtukufu, tunamuomba Mwenyezi Mungu awawezeshe nyie pamoja na walimu wenu na viongozi wenu katika kila jambo lenye heri na manufaa, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu tukuoneni mkiwa katika hali nzuri, mkiwa wahandisi, madaktari, walimu.. kila ninacho sema ni kidogo kwenu, tunamuomba Mwenyezi Mungu atujaalie sote katika kila jambo la heri”.

Viongozi wengi wameipongeza sekta ya malezi na elimu ya mkoa pamoja na Ataba tukufu kutokana na juhudi zao kwa wanafunzi, na walicho kishuhudia kwa wanafunzi wateule, wamesisitiza kua hakika wanafunzi hawa ndio viongozi wa baadae, hakika kufaulu kwa Iraq kunategemea kufaulu kwao, hafla ilihitimishwa kwa kuonyeshwa filamu yenye anuani isemayo (simulizi ya jihadi) na kugawa vyeti vya ushiriki kwa wanafunzi wateule pamoja na jopo la washiriki katika uendeshaji wa hafla hii, wakianza na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: